Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa michache ambayo yenye uoto wa asili
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa michache ambayo uoto wake wa asili haujaharibiwa.Jitihada zinaendelea kufanyika kulinda uoto huu usije kuharibiwa kutokana na shughuli za binadamu. Eneo la misitu iliyohifadhiwa ni kilometa za mraba 7,128. Kati ya eneo hilo kilometa za mraba 6,958 ni hifadhi za Taifa misitu na km 170 za mraba ni hifadhi za misitu za Halmashauri. Eneo lililohifadhiwa ni asilimia 11 ya eneo la Mkoa Katika kuyarudishia hali yake ya asili maeneo yaliyoachwa wazi baada ya kukatwa miti, katika mwaka 2007/2008 imepandwa miti 7,100,000 kati ya lengo la kupanda miti 8,000,000.Miti iliyopandwa ni miti ya asili ambayo ni migwina,mininga, miyenda na miti ya matunda. Mwaka wa 2008/2009 miche ya miti 6,900,000 imepandwa. Aidha, lengo la mwaka 2009/2010 ni kupanda miti 9,000,000 sawa na ongezeko la asilimia 30 Soma Zaidi
TAARIFA YA MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU MKOANI RUVUMA:Awali ya yote, sisi Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma tunayo furaha kubwa kuungana na Watanzania wenzetu wote katika kusherehekea mafanikio makubwa ambayo Nchi yetu imepata hadi wakati huu wa miaka 50 ya Uhuru.Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Waasisi wa Taifa letu ambao wametuongoza katika kudai Uhuru na baadae kutuwekea misingi madhubuti na imara ya Taifa letu ambayo ni Umoja, Amani, Utulivu na Mshikamano wa Kitaifa.soma zaidi
RAISI MSTAAFU WA AWAMU YA TATU Mh. BENJAMINI W. MKAPA ASHIRIKI JUBILEI YA MIAKA 25 YA ASKOFU MKUU WA KANISA LA KATORIKI RUVUMA
Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa amefaidhaishwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wanaopenda kusema kuwa watawaletea wananchi Maendeleo kwani dhana hii ni potofu na inayofifisha jitihada za .
wananchi kujiletea Maendeleo
Rais mstaafu Mh.Mkapa ameyasema hayo lwakati akitoa salamu zake katika ibada ya jubilee ya kutimiza miaka ishirini na tano ya Askofu mkuu wa Kanisa la Katoliki jimbo kuu la Songea mkoani Ruvuma soma Zaidi
Mh. Said Thabit Mwambungu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara Katika viwanja vya Nane nane vilivyopo Manispaa ya Songea .
Mh. Saidi Thabiti Mwambungu ameelezea mafanikio na changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali Mkoani Ruvuma kwa kipindi cha miaka 50 ya uhuru kwa mfano katika sekta ya Afya
"Baada ya uhuru mwaka 1961, miundombinu ya afya imeboreshwa kuanzia ngazi ya zahanati kutoka 8 hadi 197, vituo vya afya kutoka 0 mpaka 26 na Hospitali kutoka Hospital 4 hadi 10 mwaka 2011 na hivyo kuwezesha utoaji wa huduma bora za kinga na tiba kwa wananchi". Soma Zaidi