Taarifa kwa Umma
30 AGOSTI, 2018
OR-TAMISEMI, OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA INATANGAZA UZINDUZI WA KAMPENI YA FURAHA YANGU KUHAMASISHA HUDUMA ZA KUPIMA VVU NA KUANZA ARV MAPEMA.
Mkoa wa Ruvuma na wa mapambano ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI inayo furaha kutangaza uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu kimkoa.
Kampeni hii inahamasisha mkakati na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na VVU. Kupitia kampeni ya Furaha Yangu, ujumbe wa serikali ya Mkoa ni kuwakutambua hali yako ya VVU huleta amani, na kuanzishiwa ARV mapema kwa wale wenye VVU inawasaidia kuimarisha afya na kupunguza hatari ya kuambukiza VVU kwa wenza wao.
Katika kutimiza dira ya kuwa na Taifa bila UKIMWI, Tanzania imeridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90: kufikia mwaka 2020 asilimia 90 ya watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao za VVU, asilimia 90 ya watu wote wenye VVU kuanza ARV, na asilimia 90 ya wote walionza ARV kupunguza kiwango cha VVU mwilini.
Kampeni ya furaha Yangu itaanza kwa kuhamasisha wanaume wenye umri chini ya miaka 45 kujitokeza kupima VVU na kasha kuanza kuyafikia makundi mengine ya wasichana walio katika umri wa kubalehe, wanawake wenye umri mdogo ( miaka15 hadi 24), akinamama wajawazito, watu wanaotambua kuwa wanaishi na VVU na hawajaaza kutumia ARV, akinamama wanaonyonyesha na wanaoishi na VVU na Watoto wao.
Sambamba na uzinduzi wa kampeni hii, mkoa utazindua mpango wa FASTA ambao watu wanaoishi na VVU kwa ridhaa yao wataunganishwa katika mpango huu na kutumiwa ujumbe kwa njia ya simu (ARAFA) na kujitathmini mwanendo wa tiba ya kila mwezi, ARV kwa usahihi na kukumbushwa tarehe za kwenda kliniki za tiba na matunzo (CTC).Mpango huu utawasaidia wale watakao kuwa ameambukizwa kuzingatia tiba
Kampeni ya furaha Yangu itazinduliwa rasmi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb),siku ya tarehe 31 Agosti 2018, . Kumekuwepo na huduma za afya bila malipo ikiwemo huduma ya upimaji wa VVU kuanzia tarehe 28 hadi 31 Agosti,2018. Mkuu wa Mkoa inatoa wito kwa wa kazi wote wa Manispaa ya Songea na Wilaya za jirani kushiriki katika uzinduzi huu na kupima afya zao.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
S.L.B 74, Songea,Simu: 025 260 22 56, Barua pepe: rasruvuma@tamisemi.go.tz
Regional Commissioner Office
Anwani ya Posta: 74 Songea
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Hatimili@2017 Ruvuma.Haki zote zimeifadhiwa