THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - PRIME MINISTERS OFFICE
   
Search the site


 .: Home
 .: Organization structure
 .: About Us & Contact
 .: Mission & Vision
 .: Project & Programs
 .: Financial Report & Budget
 .: Documents
Taarifa za idara

 .: Kilimo na Mifugo

.: Maliasili

.: Elimu

.: Afya

.: Maji

.: Ushirika

.: Biashara

.: Barabara na Majengo

.: Ardhi, Upimaji na Ramani

.: Jamii, Jinsia & Watoto

.: Kazi

.: Sheria

.: Serikali za Mitaa


Private Area
Webmail
Maoni
Download Software
FAQ & Forums

 


SEKTA YA BIASHARA

Shughuli za biashara mkoani zinaendeshwa na watu binafsi, makampuni binafsi, vyama vya ushirika, makamapuni na Taasisi za dini. Kufuatia uamuzi wa serikali wa kufuta ada za leseni kwa biashara zenye mauzo (turnover) chini ya shilingi million ishirini (20,000,000/=) na zile zenye mauzo ya shilingi million ishirini na kuendelea kulipa shilingi ishirini elfu tu. Kumewezesha wananchi wengi kujiingiza katika biashara Mkoani. Wafanyabiashara wa ngazi zote kuanzia wadogo wa kati na wakubwa wameufurahia uamuzi huu ambao umeanza kutumika kuanzia mwezi Julai 2004. Hali hii imetoa ari kwa wananchi wengi kushiriki katika biashara ili kuendesha maisha yao.

Biashara kati ya Mkoa na Nchi jirani za Malawi na Msumbuji inafanyika kwa kiwango kidogo sana. Hali hii inatokana na ubovu wa barabara kuelekea ziwa Nyasa na ukosefu wa daraja kati ya Mkoa wa Ruvuma na nchi ya Msumbiji.

VIWANDA VILIVYOPO MKOANI KATI YA MWAKA MWAKA 2005 - 2008

S/N

Idadi ya Viwanda

 

 

Idadi ya viwanda vidogovidogo.

 

 

2005

2008

2005

2008

 

11

13

37

112

VIPIMO NA MIZANI

Utangulizi:

Ofisi ya Wakala wa Vipimo ina jukumu la kuhakiki na kudhibiti vipimo vyote vinavyotumika katika biashara pamoja na bidhaa zilizofungashwa kabisa kwa ajili ya kuuzwa bila kupimwa tena.

Mafanikio.

Mpaka sasa Mkoa umefanikiwa kudhibiti vipimo 5,922.Pia elimu ya matumizi na umuhimu wa vipimo sahihi kwa wadau imetolewa ambapo pamoja na faini kwa baadhi ya wakosaji vimesaidia kupunguza upunjaji kwa wateja (walaji). Mafanikio yetu ni 94% ya lengo.

  TCCIA MKOA

Mkoa una matawi katika Wilaya zote za Mkoa huu pamoja na matawi madogo yapatayo 16 yenye wanachama wapatao 694.

Aidha huduma zinazotolewa ni pamoja na kuendesha majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kupitia baraza la Biashara la Mkoa ambalo Mwenyekiti ni Mkuu wa Mkoa na Sekretariate wa baraza hilo ni TCCIA.

Pia wanaendesha mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kituo cha Bishara.

TCCIA Ruvuma imeweza kuanzisha kituo cha mawasiliano ya biashara ambacho kimefunguliwa rasmi tarehe 14/9/2007 katika Jengo la NSSF lililoko katika Manispaa ya Songea.

UWEKEZAJI KWA UJUMLA KATIKA MKOA WA RUVUMA

Chimbuko la mkutano wa Uwekezaji wa Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Mkoani hapa tarehe 7 Oktoba,2006 liko ndani ya Mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA).

Next

Investments Opportunity

Tourism

Tele-Communications

Extra Information

Forest Tourist Telephone Maps of Road Network
Mining Postal Services GDP
Fishing Honey Produce and Processing Radio Call Stations

Energy Sector

Industry Wildlife National Television Channels and Access Air-Plan

 


Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, P.O.BOX 74, Songea, TEL: 025 - 2602238/2602256,2602641, FAX: 025-2602144

[Go Home][WebMaster ]