
Kufuatia ongezeko la ujenzi wa madarasa Mkoa wa Ruvuma umeweza kuongeza uandikishaji wa watoto kwenda shule ya msingi kwa asilimia 106 Mwaka 2008
Ujenzi wa nyumba za walimu Shule za Msingi 2005-2008
Kuwepo nyumba bora za walimu ni moja ya motisha kwa walimu. Nyumba za walimu zilizokuwepo kufikia Desemba 2008 ni 2,507, ikilinganishw ana nyumba 2001 zilizokuwepo mwaka 2005 sawa na ongezeko la nyumba 506 ambalo ni asilimia 25.3
Nyumba za walimu shule za msingi mwaka 2005 – 2008
MWAKA |
IDADI YA SHULE |
IDADI YA WALIMU |
IDADI YA NYUMBA ZA WALIMU |
MAHITAJI |
|
MAHITAJI |
WALIOPO |
UPUNGUFU |
MAHITAJI |
WALIOPO |
UPUNGUFU |
2005 |
668
|
6696 |
5331 |
1165 |
6696 |
2001 |
4695 |
2006 |
680
|
7184 |
5699 |
1485 |
7184 |
2357 |
4827 |
2007 |
700 |
7351 |
5733 |
1532 |
7351 |
2507 |
4844 |
2008 |
723 |
7457 |
5795 |
1908 |
7457 |
2507 |
4950 |
Chanzo : Fomu za Takwimu za shule za Msingi – TSA 1 na 2 kutoka Wilayani
Elimu ya Sekondari:
Mkoa kwa kushirikiana na wananchi, Serikali Kuu pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule za sekondari. Kutokana na jitihada hizo Mkoa umeongeza idadi ya shule za sekondari kutoka shule 79 zilizokuwepo mwaka 2005, hadi shule 144 mwaka 2008 (Shule 121 za Serikali na shule 23 shule zisizo za kiserikali)
Idadi hiyo inaonyesha ongezeko la shule 65 au sawa na ongezeko la asilimia 82.3. Shule hizo zina jumla ya wanafunzi 16,113 kwa mwaka 2007, ikilinganishwa na wanafunzi 6,085 waliokuwepo mwaka 2005 sawa na ongezeko la asilimia 165. Mwaka 2008, Mkoa umefanikiwa kuwaingiza wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba, ambao idadi yao ni 12,488.
Mafanikio katika Sekta ya Elimu.
Ongezeko la uandikishaji wanafunzi shule za msingi kutoka 266788 mwaka 2005 kufikia wanafunzi 281062 mwaka 2008
Ongezeko la shule za msingi 55, kutoka shule 668 mwaka 2005 kufikia shule 723 Desemba 2008
Ongezeko la shule za sekondari za Serikali kutoka shule 79 mwaka 2005 kufikia shule 144 Desemba 2008 sawa na ongezeko la asilimia 82
Ongezeko la wanafunzi walioingia kidato cha I kutoka wanafunzi 6,085 mwaka 2005 kufikia wananfunzi 12,488 mwaka 2008 na 19,085 mwaka 2009.
Uwezo wa mkoa kudahili wanafunzi waliofaulu kufikia asilimia 100 ya waliofaulu mwaka 2008 na 2009.
Back