THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - PRIME MINISTERS OFFICE
   
Search the site


 .: Home
 .: Organization structure
 .: About Us & Contact
 .: Mission & Vision
 .: Project & Programs
 .: Financial Report & Budget
 .: Documents
Taarifa za idara

 .: Kilimo na Mifugo

.: Maliasili

.: Elimu

.: Afya

.: Maji

.: Ushirika

.: Biashara

.: Barabara na Majengo

.: Ardhi, Upimaji na Ramani

.: Jamii, Jinsia & Watoto

.: Kazi

.: Sheria

.: Serikali za Mitaa


Private Area
Webmail
Maoni
Download Software
FAQ & Forums

 

 

DHANA YA JINSIA KATIKA KUBORESHA MAISHA YA MTANZANIA - UZOEFU WA MKOA WA RUVUMA

JINSI

Jinsi ni maumbile yanayotofautisha kati ya mwanamke na mwanaume. Maumbile haya mtu anazaliwa nayo na hakuna anayechagua kuzaliwa mwanamke au mwanaume. Tofauti za kimaumbile kati ya watu hawa zinaonyesha kwamba mwanamke anao uwezo wa kubeba mimba, kujifungua (kuzaa) na kunyonyesha (maziwa au matiti yake mwenyewe) vitu ambavyo mwanaume hawezi kuvifanya. Japo sasa hivi katika nchi zilizoendelea wana sayansi wanajaribu kubadilisha maumbile haya kwa njia za upasuaji, kwa kawaida maumbile hayabadiliki.

  JINSIA.

Jinsia ni mahusiano ya kijamii yanayotambua wavulana na wasichana, wanawake na wanaume wamelelewa katika misingi tofauti kufuatana na tabia, mila, desturi, utamaduni na matarajio ya jamii husika. Mahusiano ya kijinsia yanajengwa kwa njia ya kuelekeza au kufundisha yaani makuzi na malezi au kwa mtu kujifunza. Kwa hali hiyo, mahusiano ya kijinsia yaliyojengeka vilevile yanaweza kubadilika au kubadilishwa.

UTAWALA BORA

Utawala bora ni utawala wa kuzingatia sheria, uwazi, uwajibikaji na kushirikisha jamii katika ngazi zote. Utawala bora unachochea mabadiliko katika mitazamo mbalimbali ya jamii na utawala wa sheria. Jamii lazima itumie haki yake ya msingi katika kufanya maamuzi ya masuala mbalimbali katika kujenga utamaduni wa ushirikishwaji kwa kupitia mikutano na kamati mbalimbali zilizopo kijijini.

 

MKUKUTA

Mkakati wa kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) ni mpango wa awamu ya pili wa utekelezaji wa Mkakati wa kupunguza Umasikini (MKU/PRSP) ulioandaliwa mwaka 2000. Mkakati huu (PRSP) ulifanyiwa mapitio baada ya miaka mitatu ya utekelezaji. Lengo la kufanya mapitio ni kubaini upungufu na kuboresha mkakati ili uweze kuleta mafanikio zaidi kwa wananchi kuiwezesha uchumi wa Tanzania kukua kufikia malengo yaliyo bainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo na Pia malengo ya Milenia.

 

HALI HALISI YA MASUALA YA JINSIA MKOA WA RUVUMA.

Masual ya Jinsia Mkoani Ruvuma ni mwendelezo wa jitihada nyingi zilizofanyika katika kumkomboa mwanamke katika wimbi la ubaguzi, unyanyasaji, na ugandamizaji. Ubaguzi wa kijinsia uliibua mapungufu ya kijinsia katika maendeleo ambayo yanatokana na tofauti kati ya wanawake/wasichana na wanaume/wavulana zilizojengwa kwanye mila na desturi na sheria.

Ili kurekebisha hali hiyo, kulikuwa na dhana ya wanawake na maendeleo ambapo mkazo zaidi ulikuwa kuwakomboa wanawake kiuchumi na kifikra bila kumshirikisha mwanaume. Dhana ya Jinsia na maendeleo ina sisitiza mahusiano kati ya wanawake na wanaume katika kuboresha maisha yao wote kwa pamoja.

 

Kuhusu ushirikishwaji wanawake katika maamuzi mbalimbali, wataalamu wa Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Mkoa, Halmashauri na Kata / Mitaa wamekuwa wakiwaelimisha wanawake kwa kuwajengea uwezo wa kuongoza vikundi vya kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa kila kikundi cha kiuchumi lazima kiwe na mwenyekiti wa kikundi, katibu wa kikundi, mhasibu na wajumbe. Suala hili, limeongeza ari ya wanawake Mkoani katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya ujumbe na wenyeviti katika ngazi ya kijiji na mitaa. Mfano: Wenyeviti wa mitaa katika Manispaa ya Songea wapo 71; kati yao wanaume ni 60 na wanawake ni 11 hii ni sawa na 15.5% ya mitaa yote na jumla ya wajumbe wa Serikali ya mitaa wapo 426, kati yao wanaume wapo 230 na wanawake wapo 196 hii ni sawa na 46%.

 

Licha ya elimu inayotolewa, bado nafasi nyingi za maamuzi katika Mkoa wa Ruvuma zimechukuliwa na wanaume mfano:-

 

•  Kati ya Wabunge 7 Mkoani, wabunge wanamke ni wanne (4) sawa na 57.1% ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2000 ambao kulikuwa na Mbunge mwanamke mmoja tu (sawa na 14%,)

•  Kati ya Halmashauri za Wilaya 4, nafasi moja tu ya makamu Mwenyekiti imeshikwa na mwanawake sawa na 25%, ukilinganisha na mwaka 2000 ambapo kulikuwa na wanawake wawili (2) (sawa na 50%);

•  Kati ya Tarafa 21 Tarafa nne (4) tu zinaongozwa na wanawake sawa na 19%, ukilinganishwa na mwaka 2000 ambako kulikuwa na Tarafa 5 zilizokuwa zinaongozwa na wanawake (sawa na 24%);

•  Kati ya Kata 100, Kata zenye Maafisa Watendaji Wanawake ni 17 (sawa na 17%);

•  Kati ya Sekondari 55 Mkoani, Wakuu wa shule wanawake ni 7 (sawa na 13%).

•  Kati ya Makatibu Tawala wasaidizi wa Mkoa 4, mwanamke ni mmoja (1) na wanaume watatu (3) sawa na asilimia 25%.

 

Mkakati wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Mkoani katika kuhakikisha wanawake wanashiriki katika masuala mbalimbali ya maamuzi ni pamoja na:-

•  Kuendelea kuwahimiza wanawake kugombea nafasi mbalimbali za kuongoza.

•  Kuendelea kuwahimiza wanajamii kuwasomesha watoto wote, wa kike na wa kiume kwa usawa.

•  Kuwaelimisha wananchi kuhusu kutowaoza watoto wao mara wamalizapo shule.

•  Kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa wanawake na wanaume kuwa na nafasi sawa katika uongozi kwa lengo la kuibua fulsa zilizopo za maendeleo.

•  Kuelimisha jamii dhidi ya mila potofu zinazo kwamisha maendeleo ya wananchi

 

UHUSIANO WA DAWATI LA JINSIA NA IDARA ZINGINE (NGAZI YA MKOA NA HALMASHAURI)

Katika Mkoa wa Ruvuma madawati ya jinsia yanashirikiana na wataalamu wengine kutoka katika sekta mbalimbali katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri. Sekta hizo ni; Mipango Miji, Mazingira, Kilimo, Mifugo na Afya. Hivyo wataalam hawa wanatoa utaalamu kwa kuwashirikisha wanawake na wanaume na hiyo inawasaidia katika kuboresha maisha ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma.

 

Mahusiano haya na sekta nyingine yanalenga katika masuala ya upangaji mipango ya kuzingatia jinsia, utekelezaji wa miradi mbalimbali na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayo saidia kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

 

MIPANGO YA MAENDELEO MKOA NA HALMASHAURI INAZINGATIA JINSIA?

Mipango ya maendeleo Mkoa na Halmashauri katika Mkoa wa Ruvuma inazingatia Jinsia. Mipango ya maendeleo mkoani inashirikisha wanawake na wanaume kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.

 

Katika upangaji wa mipango ya maendeleo ya Mkoa na Halmashauri tunatumia mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD). Mfumo huu unawezesha wanawake na wanaume kushiriki katika hatua za kuandaa mipango shirikishi jamii. Unatumia zana shirikishi kutambua fursa na vikwazo vilivyopo ndani na nje ya jamii husika. Kisha, jamii inatafuta njia za ufumbuzi na kuweka vipaumbele vya mipango ya maendeleo ya vijiji/kata na wilaya, inayolenga kutekeleza Dira ya Taifa ya maendeleo 2025, kama mwongozo wa kisera wa jumla na hivyo kuwa msingi wa utekelezaji wa mkakati wa kuondoa umasikini.

 

Katika Mkoa wa Ruvuma, miradi mbalimbali inaibuliwa katika ngazi za vijiji kwa kutumia mfumo shirikishi jamii, miradi hiyo inakwenda kujadiliwa na kupitishwa katika ngazi ya kata katika kikao cha maendeleo ya kata. Kutoka ngazi ya kata miradi ya maendeleo inapelekwa katika ngazi ya Halmashauri kwa kujadiliwa na kupitishwa katika kikao cha madiwani cha Halmashauri. Miradi ya maendeleo ikipitisha katika kikao cha madiwani cha Halmashauri, miradi hiyo inapelekwa katika ngazi ya mkoa ambapo inajadiliwa na kupitishwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa na hatimae kupelekwa Bungeni.

 

Aidha katika Halmashauri kuna mfumo wa ukusanyaji wa takwimu unao zingatia masuala ya jinsia. Mfumo huo unakusanya takwimu za kila sekta na baada ya kupata takwimu hizo ndizo zinatumika katika kupanga baadhi ya mipango ya maendeleo. Mfumo huo unafahamika kwa jina la "Local Government Monitoring Data base (LGMD).

NEXT

Investments Opportunity

Tourism

Tele-Communications

Extra Information

Forest Tourist Telephone Maps of Road Network
Mining Postal Services GDP
Fishing Honey Produce and Processing Radio Call Stations

Energy Sector

Industry Wildlife National Television Channels and Access Air-Plan

 


Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, P.O.BOX 74, Songea, TEL: 025 - 2602238/2602256,2602641, FAX: 025-2602144

[Go Home][WebMaster ]