THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - PRIME MINISTERS OFFICE
   
Search the site


 .: Home
 .: Organization structure
 .: About Us & Contact
 .: Mission & Vision
 .: Project & Programs
 .: Financial Report & Budget
 .: Documents
Taarifa za idara

 .: Kilimo na Mifugo

.: Maliasili

.: Elimu

.: Afya

.: Maji

.: Ushirika

.: Biashara

.: Barabara na Majengo

.: Ardhi, Upimaji na Ramani

.: Jamii, Jinsia & Watoto

.: Kazi

.: Sheria

.: Serikali za Mitaa


Private Area
Webmail
Maoni
Download Software
FAQ & Forums

 

 

USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA KUPANGA NA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MAENDELEO

Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo. Baadhi ya shughuli ambazo wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wanashiriki katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo ni pamoja na ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari, ujenzi wa ofisi za vijiji na kata, ujenzi wa madaraja (vivuko),ujenzi wa visima na ujenzi wa zahanati. Pia wako katika kamati mbalimbali za vijiji na vitongoji kama kamati za maji, TASAF, maliasili, kamati za vijiji, kamati za MMEM, MMES n.k. Mfano: Mkoa kwa kushirikisha wananchi Me & Ke umekuwa na ongezeko la kasi ya ujenzi wa madarasa ya shule za msingi kutoka madarasa 491 mwaka 2001 hadi kufikia madarasa 699 mwezi machi 2007 na ongezeko la ujenzi wa shule za sekondari kutoka shule 59 mwaka 2005 hadi kufikia shule 119 mwaka 2007.

UWEZESHAJI WA WANAWAKE KIUCHUMI

Shughuli za Dawati la jinsia Mkoa na katika Halmashauri ni pamoja na kuratibu maendeleo ya shughuli za wanawake kwa kutoa mafunzo ya kiuchumi ya wanawake. Katika kufanikisha hilo Mkoa na Halmashauri unafuatilia na kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake (WDF) ambao umeanza kutoa mikopo toka mwaka 1995/96 kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.

 

Hali ya upatikanaji wa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) kuanzia mwaka 1996 hadi 2006 ni kama ifuatavyo:-

 

HALI YA MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE (WDF) 1995/96-2006 MKOA WA RUVUMA.

S/NO

MWAKA

VIKUNDI

FEDHA (WDF)

MAREJESHO

1.

1995/96

55

5,000,000

36.5%

2.

2003

60

16,000,000

75%

3.

2005

112

39,920,000

60%

4.

2006

120

40,000,000

85%

 

Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wanatumia pia fursa ya upatikanaji wa mikopo kutoka mpango wa kuweka na kukopa VICOBA - Suistainable Development Programme, Mbinga Community Bank (MCB) na MWASOVI. Kupitia mipango hii vimeundwa vikundi vya wanawake zaidi ya 1,514 ambavyo pamoja na kujiwekea akiba vilevile hutolewa mafunzo ya ujasiriamali, jinsia, uzazi salama na UKIMWI.

MIKOPO YA VIKUNDI

VIKUNDI

IDADI YA VIKUNDI VILIVYOKOPESHWA MIKOPO

 

2005

2006

2007

2008

Wanawake

46

57

81

Hawajakopeshwa

Vijana

17

39

47

Hawajakopeshwa

 

 

 

USHIRIKIANO NA WADAU WENGINE

Ushirikiano na wadau wengine Mkoani upo. Jinsia zote (me & ke) wananufaika na huduma za mikopo itolewazo na wadau wengine kama; benki ya NMB, CRDB na SIDO. Wadau hao wanatoa elimu ya ujasiriamali na mikopo.

Mfano:- Kwa kushirikiana na SIDO Mkoa wa Ruvuma, jumla ya vikundi 4 (vikundi 3 ke 1 me) viliweza kushiriki maonyesho ya DITF Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/06 - 08/07/2007. Vile vile kupitia maonyesho ya SIDO kanda ya kusini tarehe 25/08 - 2/09/2007 jumla ya vikundi 160 vilishiriki maonyesho hayo. Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na vikundi 100, kati ya vikundi hivyo 80% vilikuwa ni vikundi vya wanawake. Katika maonyesho hayo kulikuwa na semina mbalimbali kwa wajasiriamali kuhusu ubora wa bidhaa ambapo wajasiriamali wapatao 213 walishiriki, kati yao 170 Ke na 43 Me.

 

MAFANIKIO

Dawati la jinsia la Mkoa na Halmashauri Mkoani Ruvuma yanamafanikio yaliyoanza kupatikana nayo ni:-

  • Kuna ongezeko la wanafunzi wa kike waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2006 kati ya walioanza shule mwaka 2000 kwa asilimia 67.7, ukilinganisha na wanafunzi wa kiume ambao ni asilimia 65.4. Wanafunzi walioandikishwa mwaka 2000 walikuwa 35,489 (Me18, 071 na Ke 17,418), walio fanya mtihani ni 23,609 (Me 11,817 na Ke 11,792).
  • Elimu ya jinsia imetolewa kwenye vikundi mbalimbali.
  • Elimu ya ujasiriamali imetolewa katika baadhi ya vikundi vya kiuchumi.
  • Wanawake wameongeza kiwango cha kuomba mikopo kutoka vikundi 60 mwaka 2003 hadi vikundi 120 Mwaka 2006 katika mfuko wa maendeleo ya wanawake.
  • Baadhi ya waajiri wameanza kuelewa umuhimu wa masuala ya jinsia sehemu za kazi kwa kukubali kutenga fedha za kuboresha mazingira ya kiofisi.
  • Katika kuimarisha utawala bora, Mkoa umeboresha utendaji kazi kwa kuajiri watumishi 135 kwa kipindi cha 2000 hadi 2005 (wanaume 81 na wanawake 54), ukilinganisha na ajira sita (wanaume 5 mwanamke mmoja (1)), mwaka 1995 hadi 2000 na upandishwaji vyeo watumishi 132 (wanawake 92 na wanaume 40).

 

CHANGAMOTO

Changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Dawati la Jinsia ni:-

  • Mila na destrui zisizokemea msichana kupata mimba nje ya ndoa kwa baadhi ya makabila Mkoani.
  • Upungufu wa watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii waliopata mafunzo ya jinsia.
  • Uchache wa fedha kwa ajili ya mikopo ya wanawake.
  • Mfumo dume bado ni tatizo hasa kutokana na ugonjwa hatari wa UKIMWI.
  • Mila na destrui zinazowabagua wanawake,
  • Matumizi ya teknolojia duni vijijini.

MAPENDEKEZO YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO

Ili kukabiliana na changamoto hizo mapendekezo yafuatayo yanapendekezwa:-

  • Kuendelea kutoa mafunzo ya jinsia;
  • Kuiomba Wizara ya Maendeleo ya Jamii kusaidia kushirikiana na dawati kutafuta ufadhili, ili kupata fedha za mafunzo mbalimbali na shughuli nyingine za Dawati;
  • Kushauri uongozi kuunda Kamati ya Kuratibu masuala ya Jinsia, kutokana na idara zilizopo katika sekta Mkoani na kwenye Halmashauri;
  • Kushauri uongozi kuingiza shughuli za jinsia katika Mpango wa kazi wa Mkoa na Halmashauri na fedha itengwe kwa ajili ya kazi hiyo;
  • Kushauri uongozi juu ya umuhimu wa upatikanaji wa vitendea kazi;
  • Kufanya utafiti juu ya masuala ya jinsia;
  • Kuelimisha masuala ya jinsia na takwimu zinazozingatia uchambuzi wa jinsia.

HITIMISHO

Dhana ya jinsia inaelezea jinsi wanawake na wanaume wanavyo husiana katika nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika jamii yao. Mahusiano haya ya jinsia hutokana na mchakato wa malezi, makuzi na huimarishwa na mtu binafsi, familia, taasisi za kijamii, utamaduni na itikadi.

 

Maisha bora yatapatikana iwapo watu wote yaani wanawake na wanaume watawajibika katika kuhakikisha kuwa utaratibu wa kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini mipango ya maendeleo, unazingatia uchambuzi wa kijinsia katika ngazi zote.

 

Suala la elimu ya jinsia liendane na suala zima la kubadili tabia tulizozoea katika maisha ya kila siku kwa kushirikiana Mwanamke na Mwanaume katika kupanga matumizi ya familia, Wanawake wawe na haki za kurithi mali za waume wao wanapo fariki, vitendo vya kupigwa kwa wanawake vina hatarisha amani katika familia, kuboresha matumiza ya zana za kulimia, kujadili kwa pamoja kuhusu suala la magonjwa kama UKIMWI, suala la vijana kuhamia mijini na uharibifu wa mazingira. Hivyo, bado tuna kazi nzito ya kuelimisha jamii katika suala zima la kubadilika kifikra na kimatendo katika kuboresha maisha ya jamii nzima.

Back

Investments Opportunity

Tourism

Tele-Communications

Extra Information

Forest Tourist Telephone Maps of Road Network
Mining Postal Services GDP
Fishing Honey Produce and Processing Radio Call Stations

Energy Sector

Industry Wildlife National Television Channels and Access Air-Plan

 


Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, P.O.BOX 74, Songea, TEL: 025 - 2602238/2602256,2602641, FAX: 025-2602144

[Go Home][WebMaster ]