IDARA YA KAZI
Ofisi ya kazi ndio ofisi pekee ambayo inahudumia Wilaya zote nne Mkoani Ruvuma ambazo ni Tunduru, Namtumbo, Songea na Mbinga.
Kabla ya tarehe 20/12/2006, Ofisi ya Kazi ndiyo iliyokuwa inashughulikia utatuzi wa migogoro ya kikazi, kaguzi sehemu za kazi na uendeshaji mashauri ya wafanyakazi mahakamani. Lakini kuanzia tarehe hiyo Ofisi ya Kazi haihusiki tena na kusuluhisha migogoro wala kuendesha mashauri mahakamani bali sasa inalo jukumu moja tu yaani kufanya kaguzi sehemu za kazi. Kwa mujibu wa sheria ya Ajira na mahusiano kazini 2004 Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ndiyo yenye uwezo kisheria kusuluhisha na kuamua migogoro ya kikazi.
Hivyo migogoro yote ambayo imetokea baada ya tarehe 20/12/2006 inashughulikiwa na Tume ("C.M.A." na iliyotokea kabla yake inashughulikiwa na Ofisi ya Kazi chini ya Sheria za Kazi za zamani ambazo ni Usalama kazini, Ajira n.k.
Hii ni Tume huru ambayo inapaswa kufanya kazi zake pasipo kuingiliwa na chombo chochote. Mkoa wa Ruvuma upo kwenye kanda ya Ruvuma . Kanda hii inajumuisha Wilaya zote Mkoani Ruvuma na Wilaya ya Njombe.
|