• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Muundo wa Utawala
  • Utawala
    • Sehemu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Huduma za Sheria
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyo kamilika
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Namtumbo

Watumishi wa Umma Kuweni na Subira Ongezeko la Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa

Tarehe ya kuwekwa: February 8th, 2019


Watumishi Wa Umma Kuweni Na Subira Ongezeko La Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa


 

 

 

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa, amewataka watumishi wa umma kuwa na subira kwa sababu Serikali inaendelea na mchakato wa kuwatambua watumishi wa umma halali na kufanya ulinganifu wa mishahara katika kada mbalimbali ili watumishi hao waanze kulipwa mishahara stahiki. 

 



 

Waziri Mkuu Majaliwa ameyazungumza hayo leo (07.02.2019) Jijini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe Pascal Haonga, lililohoji juu ya ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma.

 



 

Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa mwanzoni nchi ilikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakilipwa mishahara na posho mbalimbali hivyo, ili kuwatambua watumishi halali Serikali iliamua kufanya uchunguzi na kuwagundua watumishi hao hewa.

 



 

Pia, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine wa kuwatambua watumishi wenye vyeti stahiki vya kufanya kazi mbalimbali Serikalini kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.

 



 

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa baada ya kumaliza utambuzi wa watumishi halali, Rais Dkt. Magufuli aliunda Tume ya Mishahara na Motisha kwa ajili ya kufanya mapitio ya kada zote za Utumishi wa Umma na viwango vya mishahara ili kutambua ulinganifu kati ya stahiki ya mshahara na kada husika.

 



 

"Lengo la Rais Magufuli kuunda tume hiyo ni kufanya tathmini nzuri ili kutambua weledi wa kazi, uwajibikaji na tija inayopatikana mahala pa kazi, hivyo baada ya kukamilika Serikali itatoa taarifa," alisema Mhe. Majaliwa.

 



 

Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa rai kwa Watumishi wa Umma kuendelea kuiamini serikali kwani ina nia ya dhati kuhakikisha watumishi wote wanapata haki zao stahiki vile vile mpaka sasa mjadala kati ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi unaendelea vizuri

 




Matangazo

  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018 January 24, 2019
  • Kikao cha Maandalizi ya Wiki ya Maonyesho ya Viwanda na Uwekezaji January 23, 2019
  • Orodha ya Wanafunzi waliofaulu Kidato cha Kwanza Mkoa wa Ruvuma 2019 December 17, 2018
  • Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani December 02, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Watumishi 3 Manispaa ya Songea Wasimamishwa Kazi

    February 17, 2019
  • Watumishi wa Umma Kuweni na Subira Ongezeko la Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa

    February 08, 2019
  • Ufuatiliaji wa Mapato ya Ndani kwenye Halmashauri za Ruvuma

    January 17, 2019
  • Mpokezi ya Waziri Mkuu Ruvuma

    January 03, 2019
  • Angalia zote

Video

MAAGIZO YA MKUU WA MKOA KWA WATENDAJI WAKUU NA WATUMISHI WA SERIKALI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Kurasa Mashuhuru

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Regional Commissioner Office

    Anwani ya Posta: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusha
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimili@2017 Ruvuma.Haki zote zimeifadhiwa