USHIRIKA NA MASOKO
Sehemu kubwa ya mazao makuu ya biashara hununuliwa kupitia vyama vya ushirika vya msingi. Aidha, katika juhudi za kupambana na umaskini, wananchi wamekuwa wakihamasishwa kujiunga pamoja na kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS). Kutokana na umuhimu wa taasisi hizi kwa wananchi kiuchumi, idadi yake imezidi kuongezeka. Mpaka sasa Mkoa una vyama vya ushirika 208
S/N |
Vyama vya Msingi Vilivyopo |
Vyama vya Ushirika |
Mtaji wa SACCOS |
Mikopo iliyotolewa (Tshs). |
2005 |
2008 |
1 |
Mazao |
Akiba na mikopo |
Jumla
|
2005 |
2008 |
HISA (Tshs) |
AKIBA (Tshs) |
HISA (Tshs) |
AKIBA (Tshs) |
|
2 |
114 |
84 |
208 |
168 |
208 |
322, 449,572 |
1, 388, 611,356 |
600,157,764 |
4,128,843,934 |
6,649,173,439 |
Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS)
Kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi Mkoani Ruvuma kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao hasa baada ya Serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani mwaka 2005. Idadi imeongezeka kutoka vyama 31 mwaka 2005 hadi vyama 74 hivi sasa. Hili ni ongezeko la vyama 43 sawa na ongezeko la asilimia 139. Idadi ya wanachama katika vyama hivi ni 34,013 wenye hisa zenye thamani ya Shs.580,691,728.=, Akiba Shs.1,664,447,768/= na Amana shs.735,264,866/=. Wanachama waliokuwepo mwaka 2005 walikuwa 13,572 ambao hisa zao zilikuwa Shs.243,797,527/=, Akiba Shs.704,207,024.= na Amana Shs.237,468,712.=. Pia mkoa una vikundi vingi kama vikoba ambavyo huwasaidia sana wanachama wao katika kupata mitaji.
Vyama vya Ushirika vya Mazao:
Hali ya maendeleo katika vyama vya ushirika vya mazao sio ya kuridhisha. Hii ni kwa sababu shughuli kuu ya vyama hivi ni kuwa wakala wa wanunuzi binafsi wa mazao. Katika kufanya hivyo havijaweza kukidhi matumaini ya wakulima katika kutoa bei nzuri za mazao na kuwasambazia pembejeo kwa gharama nafuu. Vyama 10 tu vya msingi ndio kwa sasa vimeweza kukusanya mazao ya wakulima na kwenda kuyauza kwenye mnada, hivyo kutoa bei nzuri kwa wanachama. Vyama hivyo tisa (9) vipo katika Wilaya ya Mbinga ambavyo ni Pilikano, Malindindo, Luwaita, Maguu, Kimuli, Kipapa, Mikalanga, Longa na Mahenge. Katika Wilaya ya Songea ni Wino.
Tunaishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuvifufua vyama Vikuu vya Ushirika kwa kulipia madeni ya mabenki ya vyama vya ushirika vya Chama Kikuu cha Ushirika cha Songea na Namtumbo (SONAMCU) na Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU). Vile vile kukisaidia chama Kikuu cha Ushirika katika Wilaya ya Tunduru (TAMCU) ambapo hivi sasa imetoa mtaalam mmoja ambaye ni Mhasibu wa kusaidia kufufua chama hiki.
|