• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SEKTA ya uvuvi

6.1.4 SEKTA YA UVUVI

Katika sekta ya uvuvi, Mkoa unategemea kupata samaki kutoka ziwa Nyasa, mito, mabwawa ya asili na mabwawa ya kufugia samaki. Hata hivyo tija itokanayo na vyanzo hivyo vya samaki haitoshelezi mahitaji ya Mkoa ambayo ni zaidi ya tani 18,000 kwa mwaka, hivyo tunapata samaki kutoka nje ya Mkoa wastani wa tani 55 kwa mwezi, ukilinganisha na wastani wa mavuno ya samaki kwenye maji ya asili tani 151.5 kwa mwaka. Watalaamu wanaendelea kuhamasisha ufugaji wa samaki kwenye mabwawa ili kukidhi mahitaji ya walaji. Aidha, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 Julai hadi 2022 Septemba jumla ya wavuvi 7,635 walisajiliwa, pamoja na vikundi 38 vya wavuvi na vikundi 4 vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMUs) vilivyopo katika mialo ya Mbamba bay, Lituhi, Ndengele na Ng’ombo. Uzalishaji wa samaki katika Ziwa Nyasa ni wastani wa tani 8,411.4 kwa mwaka zenye thamani ya Tshs. 25, 234, 200,000.00.

Mkoa wa Ruvuma una jumla ya wataalamu wa kada ya uvuvi 7 ambapo katika ngazi ya Mkoa ni mmoja (1) na nane(6) wako katika ngazi ya Halmashauri za wilaya.

Jedwali Na. 33: Wataalamu wa kada ya uvuvi kwa kila halmashauri

Halmashauri

Wanaohitajika

Waliopo

Mapungufu

Waliopo kwenye mpango wa kuajiriwa 2021/2022
Tunduru

12

1

11

0

Namtumbo

21

2

19

8

Mbinga DC

31

1

30

0

Nyasa

22

1

21

5

Songea DC

18

0

18

14

Madaba

9

1

8

0

Songea MC

5

0

5

5

Mbinga TC

14

0

14

1

Jumla 

132

6

124

33

 

6.1.4.1 Uzalishaji wa Samaki Kwenye Mabwawa

Mkoa una jumla ya wafugaji wa samaki 4,170 wenye jumla ya mabwawa 6,602 yenye wastani wa uzalishaji wa tani 847.9 kwa mwaka.

Hata hivyo, Ufugaji wa samaki ni shughuli ambayo wananchi wengi wamekuwa wakiifanya katika kuongeza kipato na lishe katika jamii inayowazunguka. Kutokana na kutotosheleza kwa samaki wanaotoka kwenye  vyanzo vya samaki vilivyopo kwenye Mkoa, wananchi wanaendelea kuhamasishwa kufuga samaki kwa tija katika mabwawa ili kuweza kukidhi mahitaji hayo kwa ajili ya chakula na kwa biashara pia.Ndani ya Mkoa kuna kituo kimoja (1) cha kuzalisha vifaranga bora vya samaki kwa ajili ya wafugaji,kituo hicho kipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Ruhila (RADC) kilichopo Manispaa ya Songea.

6.1.4.2 Fursa Katika Ufugaji wa Samaki

  • Mwamko wa wananchi  wa Mkoa kuhamasika na ufugaji wa samaki.
  • Uwepo wa vyanzo vya uhakika vya maji ikiwemo,mito, chemchem na mabwawa ya Asili/Malambo zaidi ya kumi na nne (14) katika Mkoa  yenye fursa ya ufugaji wa kupandikiza au kufuga kwa njia ya vizimba(Cage culture).
  • Uwepo wa ziwa Nyasa linalotoa fursa ya ufugaji kwa njia ya vizimba (cage culture).
  • Uwepo wa mahitaji makubwa ya samaki katika Mkoa.
  • Uwepo wa wafugaji wa samaki zaidi ya 4,170 na mabwawa ya samaki zaidi ya 6,602,wanaohitaji vyakula bora vya samaki.
  • Upatikanaji wa uhakika wa malighafi za kutengenezea chakula cha samaki.

 

Jedwali Na 34Idadi ya Mabwawa, Wafugaji na Wastani wa Hali ya Uzalishaji wa Samaki Katika Mabwawa Kwa Mwaka.

Halmashauri

Idadi ya wafugaji

Idadi ya mabwawa

Uzalishaji (tani)

Tunduru

315

463

3.90

Namtumbo

200

71

1.3

Songea M.C

955

937

7.1

Mbinga

954

1,293

8.4

Songea D.C

1,327

3,227

96.8

Nyasa

170

 225

1.4

Mbinga Mji

 215

 310

1.2

Madaba

  34

 56

1.1

JUMLA

4,170

6,602

121.20

Chanzo: Halmashauri za Wilaya, Mji na Manispaa.

6.1.4.3 Matumizi ya Zana Bora Za Uvuvi.

Katika matumizi ya zana bora za uvuvi, jitihada zimewekwa ili kujenga uwezo kwa wavuvi kutambua madhara yatokanayo na matumizi ya zana haramu za uvuvi , utoaji wa elimu juu ya matumizi ya zana bora za kisasa za uvuvi zinazokubalika kisheria, kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kuhamasisha ufugaji bora wa kisasa na wenye tija. Pamoja na kuhamasisha uwanzishwaji wa vikundi vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi BMUs (Beach Management Units) hasa katika mwambao wa ziwa Nyasa na mto Ruvuma ili rasilimali za uvuvi zitunzwe, zilindwe na ziwe endelevu.  Aidha, ujenzi wa karakana ya kuunda boti za uvuvi za kisasa katika kituo cha  Mbamba Bay umefikia hatua za mwisho za kuweka mashine.

6.1.4.4 Mikakati ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi.                                                                                       

  • Kuhimiza matumizi ya zana bora za uvuvi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ambapo hadi kufikia Septemba 2022 zaidi ya wavuvi 5,380,  wafugaji 4,159 na wadau 279 wamefundishwa njia bora za uvuvi,ufugaji bora wa samaki na utunzaji wa mazingira.
  • Kuendeleza/kuboresha ujenzi wa miundombinu ya uvuvi hasa mialo(Land stations), na katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 Wizara ya Mifugo na Uvuvi(sekta ya uvuvi) ina mpango wa kujenga mualo 1 katika kijiji cha Ng’ombo.

Kutoa elimu endelevu ya uanzishaji wa vikundi vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi(BMUs) katika mwambao wa ziwa Nyasa.

Kuhimiza uanzishaji wa vituo vya uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki, ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (cage) katika ziwa na mabwawa ya asili ili kupata mavuno mengi ya samaki yatakayofaa kwa ajili ya viwanda.

Kukijengea uwezo kituo cha maendeleo ya ufugaji samaki Ruhila ili kiweze kuzalisha vifaranga bora na vya kutosha, kwa sasa kituo kina uwezo wa kuzalisha vifaranga 1,000,000.00 kwa mwaka ukilinganisha na mahitaji ya vifaranga 3,000,000 kwa mwaka.

Kila Halmashauri kuwa na kituo cha kuzalisha vifaranga bora vya samaki ambapo vituo hivyo vitatumika pia kama mashamba darasa.

  • Kuendeleza doria za mara kwa mara ili kuzuia utumiaji na uingizaji wa zana haramu za uvuvi katika ziwa na mito pamoja na kuvikagua vyombo vyote na kuvisajili kisheria. 
  • Ujenzi wa soko la samaki lililopo Mbamba bay upo katika hatua za mwisho ili liweze kutumika.
  • Mradi wa ujenzi wa maboti 6 za kisasa za Halmashauri bado unaendelea,mpaka kufikia Septemba 2022, boti 2 tayari zimeshakamilika na zinafanyakazi.

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waangaza Namtumbo

    May 15, 2025
  • AMEUONA Mwenge Songea baada ya miaka 63 ya Uhuru

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru watingisha Manispaa ya Songea,wapitia miradi ya bilioni 1.8

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua jengo la OPD zahanati ya Jimbo katoliki Mvinga

    May 14, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.