Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inatarajia kushuhudia maboresho makubwa ya miundombinu baada ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuwasilisha mpango kabambe wa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, ukilenga kurahisisha usafiri na kuchochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.
Akiwasilisha mpango huo, Meneja wa TARURA Songea, Eng. Bakari John, alisema zaidi ya Shilingi milioni 926 zitatumika katika matengenezo na usimamizi wa barabara. Kazi zitahusisha matengenezo ya kawaida kwa kilometa 94.59, ukarabati wa maeneo korofi kilometa 22.40, matengenezo maalumu kilometa 6, pamoja na ujenzi wa madaraja mawili.Kwa upande wa maendeleo, takribani Shilingi bilioni 1.67 zimetengwa kutoka Hazina, fedha za jimbo na Tozo za Mafuta ili kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 47.5 kwa kiwango cha changarawe na kujenga daraja kubwa moja,
hatua inayotarajiwa kuboresha mawasiliano na kuongeza fursa za biashara.Eng. John pia ametoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu hiyo kwa kuepuka kutupa taka kwenye mifereji ya maji au kuziba njia za kupitisha maji, akisisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni msingi wa kudumu kwa barabara bora.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.