Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kusini, Ndg. Denis Mwoleka, akiwa na timu ya watumishi wa benki hiyo, ametembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kufanya mazungumzo na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Mary Makondo.
Katika mazungumzo hayo, wameishukuru serikali ya mkoa kwa ushirikiano wanaopata, ikiwemo fursa ya kushiriki majukwaa mbalimbali ya kuelimisha watumishi wa umma kuhusu fursa zilizopo ndani ya mkoa.
Pia, ameeleza kuwa katika Wiki ya Huduma kwa Wateja, benki hiyo imetoa madawati kwa shule katika halmashauri za Mbinga TC, Madaba DC, Songea DC na Songea MC, ikiwa ni mchango wa kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo ameipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu, hususan kupitia utoaji wa madawati kwa shule mbalimbali ndani ya mkoa wa Ruvuma akieleza kuwa hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani inaboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Pamoja na mambo mengine, ameahidi kuendeleza ushirikiano na benki hiyo ili kuibua fursa zaidi kwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla, akisisitiza kuwa CRDB imekuwa mshirika muhimu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.