Katika mwendelezo wa dhamira yake ya kuwekeza kwa jamii kupitia programu ya “KETI JIFUNZE,” Benki ya CRDB imekabidhi viti na meza 40 kwa Shule ya Sekondari Mbinga,iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuinua ubora wa elimu nchini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Kanda wa CRDB, Ndg. Denis Mwoleka, alisema benki hiyo imejikita katika kusaidia sekta za Elimu, Afya na Mazingira, ikiunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha miundombinu ya elimu nchini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Bi. Amina Seif, alitoa shukrani kwa niaba ya Serikali na jamii ya Mbinga, akisisitiza umuhimu wa utunzaji wa miundombinu hiyo ili iwanufaishe wanafunzi wengi zaidi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule, Ndg. Agapiti Kindunda, aliipongeza CRDB kwa mchango huo muhimu unaopunguza changamoto ya uhaba wa viti na meza, akiahidi kuimarisha usimamizi na malezi ya wanafunzi katika matumizi sahihi ya vifaa hivyo.
CRDB inaendelea kuthibitisha kuwa elimu bora inaanzia kwenye mazingira bora ya kujifunzia.
#CRDB #KetiJifunze #ElimuBoraKwaWote #Mbinga #TanzaniaInaendelea #SamiaNiKaziTu #CSR #MotishaYaElimu

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.