Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mh. Denis Masanja amewataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa kujitoa, bidii, uadilifu na ubunifu ili kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.
Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili, nne na sita kwa mwaka 2024/25.
Mh. Masanja aliwahimiza walimu wa shule hiyo kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kuifanya Tunduru kuwa kinara kitaaluma.
Katika hafla hiyo, walimu walioshinda walipewa vyeti vya pongezi na zawadi za fedha taslimu kwa mchango wao katika taaluma na usimamizi bora wa miradi ya ujenzi wa miundombinu mashuleni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji (W) Tunduru, Bw. Chiza Marando, aliwahakikishia walimu kuwa serikali inaendelea kutoa motisha na kutatua changamoto zao ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bi. Rudia Masatu, aliwataka walimu kufanya kazi kwa weledi, mshikamano na ubunifu ili kufanikisha malengo ya wilaya ya kufikia ufaulu wa asilimia 100
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.