Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo ameongoza kikao cha maandalizi kuelekea kufanyika kwa maonesho ya Nane Nane mwaka huu 2023.
Kupitia kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mbinga (FDC) Mkuu wa Wilaya ameendelea kuhamasisha na kutoa wito kwa wadau kutoka sekta zote binafsi na za umma kushiriki katika maonesho ya Nane Nane ngazi ya Wilaya ambayo yatafanyika Kijiji cha Amanimakolo kuanzia Agosti Mosi hadi nane 2023.
kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wataalamu wa Halmashauri, viongozi wa idara, wakala na taasisi za umma, viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya tarafa, kata hadi kijiji, wadau kutoka sekta binafsi, vyama vya ushirika, makampuni na wadau wengineo.
Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Wilaya amewaongoza wajumbe wa kikao kupitia na kujadili taarifa za kamati mbalimbali za maandalizi ya maonesho hayo kwa mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.