Katika tukio linalogusa hisia za wengi, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,mkoani Ruvuma Mheshimiwa Denis Masanja, amefika Hospitali ya Misheni Mbesa kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa waliojeruhiwa baada ya mgogoro kati ya wakulima na wafugaji usiku wa Oktoba Mosi, 2025.
Akiwa hospitalini, DC Masanja aliwapa pole wahanga na kuwatia moyo, akiwahakikishia kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha usalama na utulivu vinarejea ili wananchi waendelee na shughuli zao kwa amani bila hofu.
Vilevile, alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mikononi na badala yake kutumia njia za kisheria na majukwaa ya serikali kutatua changamoto. “Mshikamano na amani kati ya wakulima na wafugaji ndiyo msingi wa maendeleo ya Tunduru,” alisisitiza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.