Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewashukuru wananchi wa Mbinga kwa mapokezi makubwa .
Akizungumza mbele ya maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo, mjini Mbinga Dkt. Samia ameahidi kuendeleza miradi ya afya na elimu kwa kujenga shule na hospitali mpya, kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, sambamba na kuimarisha huduma za ugani kwa wakulima.
Amewahakikishia wakulima kuwa serikali itaendelea kuwapa ruzuku za pembejeo na kuwaletea masoko yenye bei nzuri ya mazao yao. Aidha, alibainisha kuwa zaidi ya nusu ya vitongoji nchini tayari vimeunganishwa na umeme, na kwamba ndani ya miaka mitano ijayo kila kitongoji kitaunganishwa.
Dkt.Samia ameahidi akichaguliwa kuanzisha mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 utakaohudumia kata nane zilizobaki mjini Mbinga, akisisitiza kuwa huduma za maji safi na salama zitaendelea kusogezwa karibu na wananchi.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.