Kwenye uso wa maji ya buluu ya Ziwa Nyasa, wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, kipo Kisiwa cha Lundo , kisiwa kidogo chenye historia nzito, uzuri wa kipekee na matumaini mapya ya utalii wa Tanzania.
Zamani, Lundo lilijulikana kama kisiwa cha waliotengwa , mahali ambapo wagonjwa wa ukoma walihamishiwa na wakoloni wa Kijerumani baada ya Vita ya Majimaji (1905–1907). Leo, kisiwa hicho kimegeuka kuwa alama ya uzima, urithi na urembo wa asili.
Kwa juhudi za serikali kupitia TAWA na wadau wa utalii, Lundo sasa ni sehemu ya Hifadhi ya Mbambabay, eneo linalohifadhi wanyamapori kama swala, sungura pori, digidigi, na ndege wahamiaji kutoka Ulaya.
Mhifadhi wa kisiwa cha Lundo Maajabu Mbogo kila mwaka kati ya Septemba na Februari — mamia ya ndege kutoka ndani na nje ya nchi wanapamba anga la kisiwa hicho na samaki wa kipekee wa mapambao wakicheza chini ya maji safi yenye uangavu wa kuvutia.
Leo hii, Lundo ni mahali pa mapumziko, na unapoweza kupata picha za ndoto zako. Ni kisiwa kinachoonesha kuwa hata maumivu yanaweza kuzaa uzuri, na historia chungu inaweza kuwa urithi wa matumaini mapya.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.