Kwa msisitizo mkubwa unaogusa kiini cha maendeleo ya wananchi, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Ruben Kwagila (MB), ametoa maagizo 10 mazito yanayolenga kuimarisha nidhamu ya fedha, usimamizi wa miradi na uwajibikaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya Shule za Sekondari Amali Lundusi na Jenista Mhagama, Kwagila alisema maagizo hayo ni mwongozo wa lazima kwa Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini.
Kwa mujibu wake, ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani yafanywe kwa nidhamu, miradi iliyopo ikamilishwe kabla ya kuanzisha mipya, na hoja zote za CAG zijibiwe kikamilifu. Alisisitiza matumizi ya mifumo ya Serikali—TAUSI, MUSE na NEST—bila kufanya miamala nje ya mifumo hiyo.
Aidha, alielekeza madeni ya wazabuni yalipwe kwa wakati, mikopo isimamiwe ipasavyo, mali za Serikali zipimwe na kupatiwa hati, na kero za wananchi zisikilizwe ngazi zote. Ukaguzi wa mara kwa mara na uzingatiaji wa maadili ya Utumishi wa Umma ulitajwa kuwa nguzo ya mafanikio.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.