Wasimamizi wa Uchaguzi kata 21 wapewa mbinu na misingi ya kazi kwa weledi na uadilifu
Mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka kata zote 21 za Jimbo la Namtumbo yamehitimishwa leo Agosti 06, 2025, yakilenga kuwajengea uwezo kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yamewawezesha wasimamizi hao kupata maarifa ya kina kuhusu sheria, kanuni na taratibu zitakazoongoza mchakato wa uchaguzi. Akifunga rasmi mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Namtumbo, Ndg. Jonah Katanga, amewataka washiriki kuzingatia viapo vyao na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwazi na uaminifu wa hali ya juu.
“Ni muhimu kila mmoja wenu afanye kazi kwa kuzingatia sheria, bila kupokea maelekezo kutoka kwa watu wasiostahili. Muwe chachu ya uchaguzi huru, wa haki na unaoaminika,” amesisitiza Ndg. Katanga.
Kwa hatua hii, Jimbo la Namtumbo limejipanga vyema kuwa sehemu ya historia ya uchaguzi bora unaozingatia misingi ya demokrasia na utawala wa sheria.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.