Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma imeanzisha mafunzo ya siku tatu kwa Wataalamu wa Afya ngazi ya msingi, hatua inayolenga kuboresha huduma za kinga, utambuzi na ufuatiliaji wa magonjwa ya wazee, magonjwa yasiyoambukiza na huduma za uzazi na wagonjwa majumbani. Mafunzo hayo, yanayofanyika Novemba 26–28, 2025, yameandaliwa kwa ushirikiano na PADI pamoja na HelpAge Tanzania.
Akizindua mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Halmashauri, Dkt. Mussa Rashid, amesisitiza umuhimu wa kuwaandaa wataalamu kukabiliana na changamoto za uzee kama udhaifu wa mwili, kupungua kwa kumbukumbu na ongezeko la NCDs kama kisukari na shinikizo la damu. Ametaka washiriki kuzingatia maadili, kutoa elimu ya kinga kuhusu magonjwa ya mlipuko na kuimarisha ujumbe wa amani katika maeneo yao ya kazi.
Dkt. Rashid amehamasisha pia kuendelezwa kwa mazoezi rafiki kwa wazee—ikiwemo ngoma za asili, kutembea na mazoezi mepesi—kama njia bora ya kuongeza ubora wa maisha na kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza.
Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza weledi, kuimarisha huduma kwa makundi maalum na kuifanya Madaba kuwa mfano wa kitaifa katika utoaji wa huduma za afya za kisasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.