• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAFUNZO ya afya moja yatakavypunguza athari za magonjwa ya milipuko

Imewekwa kuanzia tarehe: August 19th, 2022

Mafunzo ya afya moja yakamilika Mtwara

MAFUNZO ya Afya moja yaliyoshirikisha wataalam mbalimbali kutoka mikoa ya Ruvuma na Lindi yamekamilika Agosti 18 mwaka huu kwenye ukumbi wa Tiffany mjini Mtwara.

Mafunzo hayo ya siku tano yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo FAO.

Wataalam walioshiriki kwenye mafunzo hayo ni wataalam wa afya za binadamu, mifugo, maliasili, mazingira,wanyamapori na wanahabari kutoka wilaya za Namtumbo na Nyasa mkoani Ruvuma na wilaya za Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mafunzo hayo ,Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dr.Vayan Laizer amesisitiza mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha watalaam hao kufanya kazi kwa Pamoja ili kushirikiana kutatua changamoto za magonjwa ya  milipuko.

Dr.Laizer amesema mafunzo hayo yamejenga uelewa namna ya kuunda timu moja kwa Pamoja ili kukabiliana na magonjwa yanayotoka kwa Wanyama Kwenda kwa binadamu au kutoka kwa binadamu Kwenda kwa Wanyama.

“Magonjwa ya milipuko yasipodhibitiwa mapema yanaweza kuleta athari kubwa katika jamii,timu ya afya moja ikishirikiana inaweza kumlinda binadamu dhidi ya magonjwa’’,alisema Dr.Laizer.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dr.Mary Kitambi ametoa rai kwa wataalam waliopata mafunzo ya afya moja,Kwenda kwenye maeneo yao ya kazi kutoa elimu hiyo kwa wataalam ambao hawakubahatika kupata mafunzo hayo.

Hata hivyo amesisitiza timu za afya moja kufanya kazi kwa kuzingatia misingi mitatu ambayo ni kuratibu,kushirikiana na kuwasiliana kwa wakati.

Valentina Sanga Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa  amelishukuru Shirika la kimataifa la FAO kufadhili mafunzo hayo ambayo yatawawezesha watalaam Kwenda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija kubwa.

Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Dr.Khatib Ramadhan ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa na FAO kwa kuwezesha mafunzo hayo ambayo yataleta matokeo makubwa wakati  wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Agosti 18,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara June 30, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • UTARATIBU wa kupandisha hadhi barabara June 30, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KAMATI ya Siasa Ruvuma yakagua jengo la DED Mbinga

    February 08, 2023
  • MAKITA sekondari wamshukuru Rais Samia kuwajengea madarasa

    February 08, 2023
  • TARURA yatumia bilioni moja kujenga lami Mbinga

    February 08, 2023
  • NDEGE mwenye uwezo wa kusafiri Dunia nzima humpumzika ndani ya hifadhi ya Gesimasowa Ruvuma

    February 08, 2023
  • Tazama zote

Video

BARABARA ya Songea -Msumbiji kuanza kujengwa
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.