Washiriki 42 kutoka kata 21 za Manispaa ya Songea wameanza mafunzo maalumu ya usimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata, yakiambatana na kiapo cha kutunza siri, ili kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru, haki na zenye uwazi.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Songea Mjini, Bw. Hossein Mghewa, amewakumbusha washiriki uzito wa jukumu walilobeba kwa mustakabali wa Taifa, akisisitiza ufuatiliaji wa Katiba na taratibu zote za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Songea Mjini, Mh. Happiness Shilembi, amewahimiza kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kuzingatia maadili ya kazi hiyo muhimu.
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo wasimamizi wa kata ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu 2025 unafanyika kwa amani, haki na uwazi.
#Uchaguzi2025 #Songea #Demokrasia #TumeYaUchaguzi #RuvumaYetuu #MaandaliziYaUchaguzi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.