Maporomoko makubwa ya Nakatuta yanayoporomoka ndani ya msitu mnene wa Pori la Akiba Liparamba, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma sasa yanatajwa kuwa miongoni mwa vivutio adimu zaidi vya utalii Kusini mwa Tanzania. Hapa, maji ya Mto Ruvuma yanachora mwanga wa asili unaowavutia watalii na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Bugwe Burenga, Afisa Utalii wa pori hilo, Nakatuta Waterfalls ni sehemu bora kwa kupumzika, kupiga kambi na kufurahia utulivu wa mazingira. “Maporomoko haya yanaunda mandhari ya kipekee ndani ya pori la Akiba Liparamba,” anasema.
Zaidi ya vivutio, Liparamba inafungua milango kwa wawekezaji wa sekta ya malazi na kambi za wageni, fursa muhimu katika kukuza utalii wa kikanda.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.