Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi (NLUPC) wamefanya ziara katika Halmashauri ya Madaba, wilayani Songea Mkoani Ruvuma, wakitoa elimu na hamasa kuhusu umuhimu wa matumizi bora ya ardhi kwa maendeleo ya wananchi na Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume hiyo, Deoskory Kanuti, alisisitiza kuwa matumizi sahihi ya ardhi huongeza mapato ya serikali kupitia hati za umiliki na hupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
“Matumizi bora ya ardhi ni msingi wa maendeleo endelevu,” alisema Kanuti, akihimiza viongozi na wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango huo.
Hadi sasa, vijiji 4,000 pekee kati ya 12,333 nchini ndivyo vilivyopiga hatua katika mpango huo, huku vingi vikiwa vinahitaji marekebisho.
Viongozi wa Halmashauri ya Madaba wamepongeza juhudi za tume hiyo na kuahidi ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha ardhi inatumika kwa tija, usawa na manufaa endelevu kwa vizazi vijavyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.