• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MILIONI 450 kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: October 31st, 2022

SERIKALI imetoa Sh.milioni 450 kwa Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma,ili kujenga vyumba  kumi vya madarasa na shule moja ya msingi ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza  na wanaotarajia kuanza elimu ya msingi mwezi Januari 2023.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe,wakati akitoa taarifa ya  maandalizi ya ujenzi wa madarasa hayo ofisini kwake kijiji cha Lundusi kata ya Maposeni km 28 kutoka  Songea mjini.

Maghembe alieleza kuwa,kati ya fedha hizo Sh.milioni 200 zitatumika kujenga vyumba kumi vya madarasa kwenye shule za sekondari zilizoanishwa kuwa na upungufu,ambapo Halmashauri imeshaanza taratibu za awali za ujenzi madarasa hayo.

Aidha alisema,Sh.milioni 250 zitatumika kujenga shule ya msingi katika kitongoji cha Lizaboni kata ya Muhukuru mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambako  katika eneo hilo ,watoto wanalazimika kutembea umbali  mrefu kwenda shule mama ya Matama.

Alisema,Serikali ya awamu ya sita imetoa fedha hizo ikiwa ni mkakati wa kuimarisha na kuboresha sekta ya elimu hususani ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa, kwenye maeneo ambayo watoto wanalazimika kwenda vijiji vingine mbali na makazi yao  kufuata shule.

Alisema,fedha hizo tayari zipo kwenye akaunti ya serikali ya kijiji ambapo wazazi na jamii ya eneo hilo wameshaanza kazi ya ujenzi ili shule zitakapofunguliwa mwezi Januri mwakani watoto wenye sifa ya kuanza elimu ya awali na msingi wayatumie madarasa hayo.

Maghembe,ameishukuru serikali ya awamu ya sita  kutoa fedha hizo ambazo zinakwenda kumaliza tatizo la vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza na shule za msingi mwakani.Amewataka watendaji na watumishi walioteuliwa kwenda kusimamia ujenzi wa madarasa hayo, kuhakikisha  wanashiriki  na kusimamia miradi hiyo kikamilifu ili kupata thamani halisi ya fedha na kujiepusha na wizi na aina yoyote ya ubadhirifu.

Pia alisema,hadi sasa wamepokea jumla ya walimu wa ajira mpya 44 wa shule za msingi na sekondari na walimu hao wameshapangiwa kwenye vituo vyao vya kazi na wanaendelea kufanya kazi ya kuwapatia watoto elimu bora.

Katika hatua nyingine Maghembe alisema,Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 inaratajia kujenga nyumba za walimu sambamba na kuongeza matundu ya vyoo kwa kila shule ya msingi.

Alisema,hatua hiyo ni mkakati wa  Halmashauri hiyo ya kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu hasa katika shule za msingi shikizi za Lihuhu,Lunyele,Jenista Mhagama,Lizaboni na maeneo mengine.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara June 30, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • UTARATIBU wa kupandisha hadhi barabara June 30, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA alivyodhamiria kuwekeza tena kwenye elimu ya sekondari

    March 24, 2023
  • CHIFU wa Tano wa kabila la wangoni Emanuel Zulu Gama

    March 24, 2023
  • MAABARA ya kisasa katika sekondari ya Lusonga Mbinga

    March 23, 2023
  • TUFANYE utalii wa ndani tusisubiri wageni kutoka nje

    March 24, 2023
  • Tazama zote

Video

RAIS SAMIA alivyomaliza kero ya maji Songea
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.