Ruvuma imeficha moja ya maajabu makubwa ya dunia: miti iliyogeuka mawe kwa zaidi ya mamilioni ya miaka. Ndani ya ushoroba wa Selous–Niassa na Pori la Akiba Liparamba, historia ya jiolojia imeganda ardhini, ikitoa kivutio adimu kinachoweza kuibadilisha Kusini mwa Tanzania kuwa kitovu cha utalii wa kijiolojia barani Afrika.
Wataalamu wanathibitisha kuwa mabaki haya, yanayojulikana kitaalamu kama *fossilized tree trunks*, ni miongoni mwa maeneo machache sana duniani na Ruvuma ndilo eneo pekee Kusini mwa Jangwa la Sahara lenye urithi huu. Matawi, mashina na maumbo ya miti yanaonekana wazi ndani ya mawe, ushahidi wa mabadiliko ya kijiolojia yaliyohusisha madini ya silika.
Mbali na wanyamapori, eneo hili lina zaidi ya aina 2,100 za mimea na zaidi ya miti 600 adimu duniani. Hali ya kutokuguswa na shughuli za binadamu imeifanya Liparamba kuwa maabara hai ya sayansi na kivutio kikubwa cha *geotourism*.
Wataalamu wa uchumi wanakadiria kuwa endapo kivutio hiki kitaendelezwa na kutangazwa kimataifa, mapato ya Ruvuma yanaweza kuongezeka kwa kiwango kikubwa.Ruvuma ina kila sababu ya kuwa jina jipya kwenye ramani ya utalii wa dunia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.