• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma wapanda miti milioni 13

Imewekwa kuanzia tarehe: July 21st, 2021

MKOA wa Ruvuma umefanikiwa kupanda miti  milioni 13,989,636 kati ya lengo la kupanda miti milioni  17 sawa  na asilimia 82  katika kipindi cha mwaka 2020/2021.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigadia Jenerali Wilbert Ibuge, amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji  wa shughuli za mazingira  kwa Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande ofisini kwake mjini Songea.

Brigedia Jenerali Ibuge amesema,  miti 10,247,000  sawa na asilimia 73.2 imepona na Serikali ya mkoa inaendelea kuhamasisha kampeni ya kitaifa ya upandaji miti inayofanyika kila mwaka kwenye Halmashauri zote.

Aidha amesema, mkoa umekuwa ukiratibu masuala mbalimbali ya usimamizi wa sheria na utunzaji mazingira ikiwa ni pamoja na  shughuli za usafi,uhifadhi na utunzaji mazingira,lengo ni kuyafanya mazingira yawe katika hali ya usalama ili kuboresha afya za binadamu na ustawi wa viumbe hai.

Akizungumzia suala la uzalishaji  wa taka ngumu katika wilaya zote za mkoa huo amesema,takribani tani 39,596 kwa mwaka  zinazalishwa na asilimia kubwa  ni za majumbani na sehemu za biashara hasa za masoko.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa, taka zinazozalishwa majumbani udhibitiwa kwa njia za mashimo pamoja na utekelezaji  kwa moto  na  Halmashauri  zote zimeendelea kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa madampo ya kutupa taka.

Brigedia Jenerali Ibuge ameongeza kuwa, hata hivyo kutokana na ongezeko la viwango vya maisha na ukuaji wa haraka wa shughuli za maendeleo pamoja na ongezeko la watu,kumesababisha kuongezeka sana kwa uzalishaji wa taka ngumu na maji taka kutoka kwenye makazi ya watu hasa katika Manispaa ya Songea.

Mkuu wa mkoa amesema,ongezeko hilo limesababisha kuwa na uzalishaji mkubwa wa taka ambao hauendani na uwezo wa Manispaa ya Songea kuweza kukusanya taka hizo ambapo kiwango cha taka zinazozalishwa ni tani 71.5 kwa siku.

Kwa upande wake  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande, amepongeza juhudi za Serikali ya mkoa wa Ruvuma  ya kupanda miti kwa asilimia 70, na ametaka utaratibu huo uendelee mwaka hadi mwaka.

Aidha, ameagiza Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma kuhakikisha zinapanda miti takribani elfu mbili kwa mwaka ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na kuongezeka kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Ametaka,suala la  kutunza mazingira liwe kama wimbo wa kila siku kwani itasaidia sana wananchi kutambua  wajibu  na amewataka watendaji wa serikali, kushirikiana na jamii kudhibiti uharibifu wa mazingira na vyanzo vyote vya maji ili viwe endelevu kwa maisha ya binadamu na viumbe wengine.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara July 31, 2022
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma July 31, 2022
  • MKATABA wa Lishe Mkoa wa Ruvuma June 30, 2022
  • ILANI ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020/2025 August 31, 2021
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAWA Ruvuma wakamata meno ya tembo

    May 18, 2022
  • WWF yazindua elimu ya uhifadhi kwa shule za msingi Ruvuma

    May 17, 2022
  • FUKWE za Nyasa

    May 17, 2022
  • VIVUTIO vya utalii Nyasa

    May 17, 2022
  • Tazama zote

Video

MSEMAJI Mkuu wa Serikali apongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza habari mtandaoni
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.