Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Crispin Francis Chalamila ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma, ambapo amewasili katika Wilaya ya Namtumbo na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Ngollo Malenya
Lengo kuu la ziara hii ni kufuatilia utendaji wa ofisi za TAKUKURU wilayani humo, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hiyo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, na taasisi za umma, ili kuhakikisha miradi ya maendeleo na huduma za umma zinatolewa kwa ufanisi na kwa uwazi bila mianya ya rushwa.
Ziara hii inaonesha dhamira thabiti ya uongozi wa TAKUKURU kuwafikia wananchi katika ngazi zote, kuimarisha uwajibikaji, na kujenga jamii yenye uadilifu na maadili bora.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.