• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MPANGO wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu wazinduliwa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: January 23rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amesema Ruvuma ni kati ya mikoa 9 iliyokuwa na uibuaji mdogo wa wagonjwa wa kifua kikuu kwa mwaka 2024 ambapo wagonjwa 1,278 waliibuliwa kati ya lengo la wagonjwa 2,515 waliopaswa kuibuliwa.

Ameyasema hayo wakati akizindua Mpango Harakishi wa Kuibua Wagonjwa wa Kifua Kikuu uliofanyika katika uwanja wa nje ya soko kuu la Songea mjini lililopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

"Kwa Mkoa wa Ruvuma wagonjwa walioibuliwa ni asilimia 50.79 tu, hivyo bado tunalo jukumu la kuwapata wagonjwa 1,132 ambao bado wapo katika jamii tunayoishi wakiendelea kuwaambukiza watu wengine," alisema Kanali Ahmed.

Ameongeza kuwa takwimu zinadhihirisha kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ni janga kubwa na kikwazo kwa maendeleo ya Taifa kwa sababu wanaougua wanashindwa kuzalisha mali hivyo kutochangia vizuri katika pato la Taifa na kumudu maisha yao wenyewe.

Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dr. Jacob Mwanamtwa, amebainisha kuwa kampeni hiyo ilianza Januari 20, 2025 na hadi kufikia Januari 22 wamefanikiwa kukusanya sampuli kwa wagonjwa 851 na waliogundulika kuwa na ugonjwa huo na kuanza matibabu ni 24 sawa na asilimia 2.8.

Amelitaja lengo la kampeni hiyo ni uharakishaji wa uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu waliokosekana mwaka 2024 ili kuweka jitihada kwa pamoja na umoja katika kupambana na kifua kikuu, kuboresha na kuharakisha ufanisi wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori, amesema kifua kikuu ni moja ya magonjwa yanayoambukizwa  ambayo ni tishio hivyo wataendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali wanaoratibu shughuli hiyo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile, amesema Tanzania ni moja kati ya nchi 30 zinazokabiliwa na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu hivyo amewashauru wananchi wa wilaya wa Songea kukata bima ya Afya ili ziwasaidie hata wanapopata tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu wawe na uhakika wa kutibiwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2024 kulikuwa na wagonjwa milioni 10.8 wa kifua kikuu duniani kote, kati yao milioni 1.25 sawa na asilimia 12 walifariki kutokana na ugonjwa huo, Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya laki 122,000 sawa na wagonjwa 183 kwa kila watu 100,000 walioibuliwa na kuanzishiwa dawa ni 92,720 sawa na asilimia 76.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • AMEUONA Mwenge Songea baada ya miaka 63 ya Uhuru

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru watingisha Manispaa ya Songea,wapitia miradi ya bilioni 1.8

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua jengo la OPD zahanati ya Jimbo katoliki Mvinga

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua mradi wa jengo la OPD zahanati ya Jimbo Katoliki Mbinga

    May 14, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.