Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, amewasili mkoani Ruvuma kwa ziara ya kichungaji na kijamii ambapo pamoja na mambo mengine amesema watazungumza na jamii kuhusu mmomonyoko wa maadili na utunzaji wa amani.
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, ofisini kwake mjini Songea, Sheikh Zubeir amesisitiza kuwa katika ziara hiyo wamelenga kutoa elimu kuhusu mmonyoko wa maadili ambalo limekuwa ni tatizo kubwa katika jamii.
Vilevile amesema watazungumza na kuhimiza kuhusu umuhimu wa kutunza amani katika taifa akisisitiza kuwa ni tunu adhimu aliyoijalia Mwenyezi Mungu kwa taifa la Tanzania.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amemkaribisha Sheikh Abubakar Zubeir kwa heshima, akieleza kuwa hali ya kidini na kisiasa katika mkoa huo ni ya utulivu na mshikamano.
Amesisitiza kuwa kuna ushirikiano mzuri si tu kati ya serikali na taasisi za kidini, bali pia miongoni mwa taasisi za kidini zenyewe, jambo linalochangia kudumisha amani na kuimarisha maendeleo ya jamii.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.