• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWAMBAO wa ziwa Nyasa utakavyounganishwa barabara ya lami Lituhi hadi Chiwindi

Imewekwa kuanzia tarehe: May 18th, 2020

SERIKALI inatarajia kuunganisha kwa mtandao wa lami mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma kuanzia Lituhi hadi Chiwindi mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema serikali imetoa shilingi bilioni 129 za ujenzi wa lami nzito yenye urefu wa kilometa 66 toka Mbinga  hadi Mbambabay makao makuu ya wilaya ya Nyasa ambapo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 50.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mtupale wilayani Nyasa,Mndeme amesema katika bajeti ya mwaka huu serikali imeingiza kwenye bajeti barabara yenye urefu wa kilometa 41 kuanzia Nang’ombo hadi Chiwindi mpakani na nchi ya Msumbiji.

“Katika mwaka huu tumeweka kwenye bajeti ya fedha barabara hii ifanyiwe usanifu na upembuzi yakinifu ili ijengwe kwa kiwango cha lami’’amesema Mndeme.

Ametoa rai kwa wananchi wakiona watalaam wa barabara wanafika kupima kutoa ushirikiano na kwamba ukarabati unaofanyika kwenye madaraja katika barabara hiyo ni kuwezesha magari kupita katika kipindi hiki cha mpito.

Amesema usanifu na upembuzi yakinifu katika barabara ya Kitai,Lituhi hadi Mbambabay umekamilika na kwamba kinachosubiriwa ni kutenga bajeti ili ujenzi wa barabara uweze kuanza hali ambayo itawezesha wilaya ya Nyasa kuunganishwa na mtandao wa lami.

Mndeme ameongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kuwa wananchi wa Nyasa wanaepukana na  changamoto ya usafiri na usaifirishaji ambapo tayari serikali imenunua meli tatu ,mbili za mizigo na moja ya abiria  na kwamba wakazi wa Nyasa ndiyo watakaonufaika zaidi ya usafiri wa meli hizo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amewataka wananchi  wa Kata ya Chiwanda wilayani Nyasa waliopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji  kulinda Nchi ya   Tanzania kwa niaba ya Watanzania wengine ili kuhakikisha nchi  inakuwa salama kutokana na kwamba serikali itajenga barabara hiyo ili kuimarisha usalama.

Kuunganishwa kwa mtandao wa lami katika wilaya ya Nyasa kutaufanya Mkoa wa Ruvuma kuunganishwa kwa barabara ya lami katika ukanda wa Mtwara korido kuanzia Mtwara hadi Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Mei 18,2020

Matangazo

  • RATIBA ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 October 14, 2023
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara December 31, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatangaza kufunga rasmi mfumo wa ununuzi wa TANePs Septemba 30 mwaka huu

    September 23, 2023
  • MKUU wa Mkoa alivyomkabidhi Mkakati wa Utalii Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma

    September 23, 2023
  • CHIFU wa Wangoni alivyokabidhiwa Mkakati wa Utalii Mkoa wa Ruvuma

    September 23, 2023
  • MKUU wa Wilaya ya Tunduru azindua Jukwaa la Wanawake wa Tunduru

    September 23, 2023
  • Tazama zote

Video

WAZIRI APONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA HALMASHAURI YA MADABA
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.