Mkoa wa Ruvuma wapo mbioni kushuhudia operesheni kubwa ya kitaalamu ya uchunguzi wa kifua kikuu (TB) kwa wachimbaji wa madini na jamii zinazozunguka migodi, kuanzia Oktoba 6 hadi 10!
Kampeni hii maalum inaratibiwa na Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Ambukizi ya Kibong’oto kwa ushirikiano na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma, ikilenga kuwalinda wachimbaji dhidi ya athari za vumbi la silica na magonjwa sugu ya mapafu.
Akizungumza katika kikao kazi cha wataalamu wa afya mjini Songea, Mkuu wa Mkoa Brig. Jen. Ahmed Abbas Ahmed ametoa rai kwa wataalamu “kujitoa kikamilifu ili kulinda afya za jamii zetu.”
Tanzania inatajwa na WHO kuwa miongoni mwa nchi 30 zenye mzigo mkubwa wa TB duniani – zaidi ya watu 130,000 huathirika kila mwaka.
Kwa upande wake, Dkt. Leonard Subi, Mkurugenzi wa hospitali ya Kibong’oto, amesema watatumia Kliniki Tembezi (Mobile Clinic) kufika moja kwa moja migodini, kutoa uchunguzi bure, elimu ya afya, na dawa papo hapo kwa watakaobainika kuwa na TB.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.