Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya amesema Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limejipanga kuhakikisha usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu Ili wananchi washiriki bila hofu yoyote.
Kamanda Chilya ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma.
"Kuelekea uchaguzi Mkuu jeshi la polisi mkoani Ruvuma limejipanga kusimamia usalama kabla, wakati na baada ya uchaguzi" Alisema.
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 utakaohusisha nafasi ya Rais, wabunge na madiwani, utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.