Katika kuadhimisha miaka 14 ya kulitumikia taifa, Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma wameamua kusherehekea kwa njia ya kipekee kwa kugusa maisha ya watoto wenye uhitaji.
Wakiongozwa na Mkaguzi wa Polisi Koladina Mahundi, askari hao wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya TSh 500,000 kwa Kituo cha Watoto Wenye Usonji kilichopo Shule ya Msingi Subira, Manispaa ya Songea.
“Ni utamaduni wa Jeshi la Polisi kuwafariji watoto wenye uhitaji,” alisema INSP Mahundi, akitoa wito kwa taasisi binafsi, wafanyabiashara na wananchi wote kutembelea vituo vya kulelea watoto yatima na kutoa msaada, ili watoto hao wajue hawajasahaulika.

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.