Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Mary Makondo, ameagiza kuongezwa kwa kasi ya usimamizi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mpandangindo, wilayani Songea, ambacho serikali imetoa Tsh milioni 250 kukamilisha mradi huo muhimu kwa wananchi.
Makondo alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, akisisitiza uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma.
Aidha, ameagiza mamlaka zote za serikali mkoani Ruvuma ikiwemo shule, vituo vya afya na ofisi za umma kuhakikisha zinakuwa na hati miliki ili kulinda mali za serikali na kuzuia migogoro ya ardhi.
Wakati huo huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo amekagua mradi wa ukarabati wa shule ya msingi Mpandangindo katika Halmashauri ya wilaya ya Songea ambapo serikali kupitia program ya BOOST imetoa shilingi milioni 100 kutekeleza mradi huo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.