Mradi wa ukamilishaji wa miundombinu ya Shule ya Msingi Shikizi Lilambo B Manipspaa ya Songea mkoani Ruvuma umeingia katika hatua ya mwisho, ukigharimu shilingi milioni 32.2, ikiwa ni juhudi za Serikali na Halmashauri kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa eneo hilo.
Akitoa taarifa kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, aliyefanya ziara ya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali katika Manispaa ya Songea, Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Marthai Lipa, alisema fedha hizo zinatokana na vyanzo viwili ambapo shilingi milioni 25 zikitolewa na Serikali Kuu, huku shilingi milioni 7.2 zikitokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mwalimu Martha alieleza kuwa fedha hizo zimetumika kukamilisha vyumba viwili vipya vya madarasa, kukarabati vyumba viwili vya madarasa vya zamani, kujenga ofisi moja ya walimu, na kununua madawati ya walimu .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Makondo, ameridhishwa na hatua iliyofikiwa, akiwapongeza walimu na kamati ya shule kwa usimamizi bora wa fedha na utekelezaji wa mradi huo kwa uwazi.
Shule ya Msingi Shikizi Lilambo B, ambayo ina zaidi ya wanafunzi 700, imekuwa ikikabiliwa na changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa na miundombinu chakavu kwa miaka kadhaa. Kupitia mradi huu, changamoto hizo zinatarajiwa kupungua kwa kiasi kikubwa, huku walimu na wanafunzi wakitarajia kuanza kutumia vyumba vipya kabla ya mwisho wa mwaka huu..
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.