• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE aagiza mbolea mkoani Ruvuma kuuzwa kwa bei elekezi

Imewekwa kuanzia tarehe: March 18th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amefanya ziara ya ukaguzi wa maghala ya kuhifadhia mbolea yaliyopo Manispaa ya Songea.

Akizungumza katika ziara hiyo ameagiza kuanzia sasa wafanyabiashara wafuate bei elekezi ya mbolea ambayo ni  shilingi laki moja na elfu tano na kwamba kuuza mbolea hizo kwa bei ya juu ni kinyume cha sheria.

RC Ibuge ameagiza wananchi wote waliolipishwa mbolea kwa bei ya 138,000 kwa mfuko wa kilo 50 warejeshewe fedha zao kwenye maduka ambayo walinunua mbolea hizo ‘’,alisisitiza.

Amesisitiza kuwa kupanda kwa bei ya mbolea kunatokana na kuagiza toka nje ya nchi na kwamba dunia nzima inahitaji mbolea hizo  hivyo bidhaa inapotakiwa na wengi bei inapanda na kwamba sio kweli kwamba serikali imepandisha bei.

Hata hivyo amesema serikali imeweka mpango mzuri wa  wa kitoa kibali kwa waagizaji ambao wanaleta mbolea nchini na kwamba katika Mkoa wa Ruvuma kuna maghala ya kutosha ya kuhifadhia mbolea za aina mbalimbali.

Hata hivyo amesema kuanzia msimu ujao wa kilimo bei ya mbolea nchini inatarajiwa kushusha kutokana na serikali kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea za aina mbalimbali jijini Dodoma.

Pia, RC Ibuge amesikiliza kero za wananchi wa Mtyangimbole na amewataka waache ubaguzi na matabaka baina yao juu ya umiliki wa ardhi kwani wote ni Watanzania hivyo wawe na umoja.

‘’Kila mamlaka iwe ya Kijiji au Halmashauri ina jukumu la kupanga mipango bora ya ardhi ya kijiji iko ili kuondoa matabaka na migogoro isiyo ya lazima ‘’, amesema RC Ibuge.

Aidha, amesema ni jukumu na ni wajibu wa serikali Tanzania pamoja na Vijiji vyake vyote viwe vimefikiwa umeme ifikapo Desemba 2022 hivyo wananchi wa Mtyangimbole wasiwe na wasiwasi katika swala la umeme.

Nae Mzee Komba mkazi wa Mtyangimbole amemuomba Mkuu wa Mkoa wakati  wanapokuja kununua mahindi wakulima washirikishwe kwenye upangaji wa bei kwasababu wao ndio wanajua mahindi yamezalishwaje pamoja na gharama.

Mkoa wa Ruvuma kwa miaka mitatu mfululizo umekuwa kinara wa kuzalisha chakula nchini.

Imeandikwa na Bahati Nyoni

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Machi 18,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara June 30, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • UTARATIBU wa kupandisha hadhi barabara June 30, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENYEKITI CCM Mkoa wa Ruvuma akipanda Mti

    February 03, 2023
  • MAJENGO ya Zahanati ya Kipingo-Madaba

    February 03, 2023
  • Ruvuma ya kijani

    February 03, 2023
  • Ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa Songea-DC

    February 02, 2023
  • Tazama zote

Video

BARABARA ya Songea -Msumbiji kuanza kujengwa
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.