• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE aagiza usimamizi makini miradi ya madarasa ya UVIKO

Imewekwa kuanzia tarehe: November 30th, 2021

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Balozi Wilbert Ibuge,amewaagiza wasimamizi wa miradi ya ujenzi ya vyumba vya mdarasa inayotekelezwa kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na  mapambano  dhidi ya Uvico-19 kuwa makini na matumizi ya fedha.

Balozi Ibuge alisema, ni vema kila hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo kuwa na utaratibu wa kupiga picha ya hali halisi ili  kudhibiti udanganyifu unaoweza kufanywa na wasimamizi wasio waaminifu kwa lengo la kutafuta maslahi binafsi.

Ametoa kauli hiyo jana wakati akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ruanda Halmashauri ya wilaya Mbinga vinavyojengwa kupitia fedha za mpango wa  maendeleo ya kwa Taifa na mapambano dhidi ya Uvico-19.

Alisema,ni vizuri kila hatua ya utekelezaji wa miradi ya  maendeleo sio kwa inayojengwa kupitia fedha za Uvico 19 tu,bali hata miradi mingine inayotekelezwa katika mkoa huo ipigwe picha ili  kuepuka udanganyifu unaoweza kufanywa na mafundi na wasimamizi wa miradi husika.

“kuanzia sasa nataka tubadilike katika suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huu,nahitaji kila hatua lazima mradi upigwe picha ili kutusaidia kufahamu ubora wake na kama unalingana na thamani ya fedha zilizotolewa”alisema Balozi Ibuge.

Amewataka wataalam wa ngazi mbalimbali katika mkoa huo, kushirikiana na kusimamia kazi ya ujenzi wa miradi hiyo ili iwe na ubora na kuleta tija kama ilivyokusudiwa ya kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 wanapata nafasi kwenye shule walizopangiwa.

Akiwa katika Halmashauri ya wilaya Mbinga,Ibuge alitembelea shule ya Sekondari Ruanda,Mkako,Shule ya Wasichana Mbinga na Kihamili kwa ajili ya kukagua  ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarasa katika shule hizo na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Juma  Haji ameishukuru Serikali kwa kuipatia shule ya sekondari Ruanda  sh.milioni 40  ili kujenga vyumba viwili vya madarasa ambayo yanajengwa kwa mfumo wa force akaunti na  fedha zilizotumika hadi sasa ni Sh milioni 12.

Alisema, hadi sasa kazi zinazoendelea katika ujenzi huo ni kupiga ripu,kupachika grill na kuezeka na  kazi hiyo itakamilika kabla ya tarehe 10 Desemba mwaka huu.

Akiongea kwa niaba  ya Wanafunzi wenzake Miriam Komba wa kidato cha tatu,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa uamuzi wa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Alisema, kujengwa kwa madarasa hayo kutamaliza changamoto ya upungufu wa madarasa kwa wanafunzi wa shule hiyo na hivyo kuwa na matumaini ya kufanya vizuri kitaaluma.

Hata hivyo,ameiomba Serikali kutatua changamoto kubwa ya huduma ya maji safi na salama kwani licha ya shule hiyo kuwa na miundombinu ya maji,lakini hayapatikani mara kwa mara badala yake wanalazimika kutumia maji ya mto Tip Tip ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu.

Imeandikwa na Muhidin wa Amri mgazeti ya serikali Ruvuma

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • AMEUONA Mwenge Songea baada ya miaka 63 ya Uhuru

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru watingisha Manispaa ya Songea,wapitia miradi ya bilioni 1.8

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua jengo la OPD zahanati ya Jimbo katoliki Mvinga

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua mradi wa jengo la OPD zahanati ya Jimbo Katoliki Mbinga

    May 14, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.