• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC MNDEME awasimamisha TBA ujenzi jengo la Halmashauri ya Madaba,TAKUKURU kuchunguza

Imewekwa kuanzia tarehe: June 7th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewasimamisha Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuendelea na ujenzi jengo  la Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Mndeme amechukua uamuzi huo baada ya TBA kushindwa kukamilisha mradi huo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,licha ya serikali kutoa zaidi ya shilingi bilioni 2.2 za utekelezaji wa mradi huo.

“Mimi silei wabadhirifu na wahujumu,Kuanzia leo hatuwaongezei tena muda,kuanzia sasa TBA,msimame ujenzi wa jengo hili na ujenzi wake utaendelea kwa kutumia force account,pia naagiza kuanzia leo TAKUKURU waanze kuchunguza mradi huu’’,alisisitiza Mndeme.

Mndeme amewaagiza TAKUKURU kuchunguza sababu za mradi huo kusuasua na kuchukua muda mrefu na kwamba iwapo kuna mtu yeyote amefanya hujuma dhidi ya mradi huo achukuliwe hatua haraka.

Amesisitiza haiwezekani jengo moja linachukua miaka zaidi ya mitatu hali ambayo inachelewesha maendeleo ya eneo husika,amelitaja lengo la Rais kutoa fedha hizo ni kutaka kuona watumishi wanafanyakazi katika mazingira rafiki na wananchi wanapata huduma katika mazingira bora.

Amewataka TBA wanapoomba kazi,kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati ambapo amesema licha ya kuongezewa muda wa mkataba mara mbili,bado wameshindwa kukamilisha mradi huo.

Amewatahadharisha TBA wasihangaike kuomba kazi za ujenzi ndani ya Mkoa wa Ruvuma kwa sababu miradi yote waliokuwa wanatekeleza ndani ya Mkoa wa Ruvuma wameshindwa kukamilisha.

Mndeme amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea kuhakikisha anasimamia mradi huo wakati,ambao sasa unakamlishwa kwa force account kwa wakati na viwango na kwamba serikali hivi sasa inatekeleza kwa wakati na viwango miradi mingi kwa force account.

Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi huo kutoka kampuni ya BICO Ahmed Nyange  amesema mradi huo ambao umefikia asilimia 84 ulitarajiwa kukamilika Januari 20 mwaka huu,ambapo Mkandarasi aliongezewa miezi minne hadi Mei 31 mwaka,pia ameshinda kukamilisha mradi.

Nyange amesema hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa zaidi ya shilingi bilioni moja sawa na asilimia 61 ya gharama yote ya mradi na kwamba mkandarasi ameshindwa kukamilisha mradi kwa wakati ambapo amesema BICO inaunga mkono kukamilisha mradi kwa force account.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Shafii Kassim Mpenda amesema TBA imekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zinajitokeza mara kwa mara na kusababisha mradi kushindwa kukamilika kwa wakati.

“Nasikitika kusema kwamba imebidi tufikie hapa tulipofika ili kunusuru mradi na fedha za umma  tusitishe mkataba na TBA na tuombe ridhaa kutoka kwa Katibu Mkuu wa TAMISEMI ili aridhie kukamilisha kazi zilizobaki kwa kutumia force account.

Awali Mwakilishi wa TBA Mhandisi Elias Tillya alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwa walianza vizuri utekelezaji wa mradi huo na walitarajia Juni mwaka huu kukabidhi jengo hilo.

Hata hivyo amesema mwishoni mwa Mei mwaka huu TBA ilipata changamoto kwenye akaunti zake katika mikoa yote nchini hali ambayo ilisababisha kushindwa kutoa fedha baada ya akaunti zake zote kuzuiwa.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 6,2020

Madaba

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara July 31, 2022
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma July 31, 2022
  • MKATABA wa Lishe Mkoa wa Ruvuma June 30, 2022
  • ILANI ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020/2025 August 31, 2021
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAWA Ruvuma wakamata meno ya tembo

    May 18, 2022
  • WWF yazindua elimu ya uhifadhi kwa shule za msingi Ruvuma

    May 17, 2022
  • FUKWE za Nyasa

    May 17, 2022
  • VIVUTIO vya utalii Nyasa

    May 17, 2022
  • Tazama zote

Video

MSEMAJI Mkuu wa Serikali apongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza habari mtandaoni
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.