Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amekagua ujenzi wa daraja la dharura katika Mto Mnywamaji, Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga, kufuatia agizo la Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, alilotoa Desemba 21.
Katika ziara hiyo, RC Ahmed amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri na ambapo wataalamu wamemthibitishia kuwa daraja hilo la dharura litaanza kutumika Janauari 1, 2026.
Ametoa rai kwa wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha daraja la kudumu na kuzuia kukatika kwa mawasiliano katika eneo hilo ili shughuli za kijamii na kiuchumi ziendelee.
Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Amani Makolo - Ruanda, Mhandisi Andrew Sanga, amethibitisha kuwa daraja hilo liko katika hatua za mwisho za ukamilishaji. Amesema ifikapo Januari 1, 2026 daraja litaanza kutumika rasmi, na hivyo shughuli za kiuchumi ambazo zilisimama kwa muda, ikiwemo usafirishaji wa makaa ya mawe, zitaendelea kama kawaida.
Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga, Protasi Mapunda, ameiomba serikali kuiangalia barabara hiyo ya Amani Makolo - Ruanda na kuifanyia ujenzi ili kupunguza adha ya ubovu wa miundombinu ya barabara kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.