Katika kampeni zake mjini Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango kabambe:
“Tuko kwenye mazungumzo kwamba tuweze kujenga reli kwa viwango vya kisasa kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay. Ni wazi kwamba reli hii tukiweza kuijenga itaambatana na manufaa makubwa sana ya kiuchumi kwa ukanda huu wa Kusini.”
FURSA MPYA ZA UCHUMI
Reli hii ikikamilika itarahisisha:
• Usafirishaji wa bidhaa na mazao ya kilimo kutoka Kusini.
• Ufunguzi wa masoko mapya ya ndani na nje ya nchi.
• Uwekezaji mkubwa katika viwanda na biashara.
KUSINI KUINUKA
Mradi huu unatazamiwa kuimarisha nafasi ya ukanda wa Kusini kama kitovu cha uchumi, biashara na ajira, huku ukichochea maendeleo endelevu kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.