• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RUVUMA ilivyodhamiria kupambana na malaria

Imewekwa kuanzia tarehe: April 22nd, 2025

Katika mkoa wa Ruvuma, ugonjwa wa malaria bado unaendelea kuwa changamoto kubwa ya kiafya, licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa kudhibiti maambukizi yake. 

Kwa miaka mingi, malaria imekuwa chanzo kikuu cha wagonjwa hospitalini na hata vifo, hasa miongoni mwa watoto na kina mama wajawazito.

Kulingana na matokeo ya tafiti za Malaria  zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kiwango cha maambukizi ya malaria mkoani Ruvuma kimeshuka kutoka asilimia 11.8 mwaka 2018 hadi asilimia 7.9 mwaka 2022. 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Louis Chomboko anasema Kushuka huku ni hatua muhimu, kwani kiwango hicho kiko chini ya wastani wa kitaifa wa asilimia 8.1 kwa mwaka 2022.


Maeneo Yenye Maambukizi Juu na Chini

Ingawa kiwango cha jumla kimepungua, baadhi ya halmashauri bado zina viwango vya juu vya maambukizi. 

Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo inaongoza kwa asilimia 16, ikifuatiwa na Wilaya ya Tunduru yenye asilimia 15,vikiwa ni viwango maradufu ya wastani wa kitaifa. 

Kwa upande mwingine, Halmashauri ya Mji wa Mbinga na Manispaa ya Songea zimeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa na viwango vya chini vya maambukizi ya asilimia 5 


Mikakati Madhubuti ya Kupambana na Malaria

Katika kutekeleza mpango wa kudumu wa kutokomeza malaria, Mkoa wa Ruvuma unaendesha kampeni chini ya kauli mbiu ya kitaifa: “Ziro Malaria Inaanza na Mimi”. 

Mpango huu unalenga kuhusisha kila mwananchi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu kwa njia mbalimbali.

Mojawapo ya mikakati hiyo ni ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia programu ya School Net kwa wanafunzi mashuleni, pamoja na programu ya Chandarua Clinic kwa wajawazito na watoto wachanga kwenye vituo vya afya. 

Hadi kufikia Desemba 2024, Mkoa wa Ruvuma ulikuwa umesambaza jumla ya vyandarua 363,378, ambapo 167,396 vilitolewa kupitia Chandarua Clinic na 195,982 kupitia School Net.


Udhibiti wa Mbu: Mazingira na Teknolojia

Mbali na ugawaji wa vyandarua, Mkoa pia umeimarisha mapambano kwa kutumia mbinu ya upuliziaji wa viuadudu kwenye mazalia ya mbu. 

Mwaka 2024 pekee, jumla ya lita 1,200 za viuadudu zilitumika kupulizia mazalia ya mbu katika halmashauri mbalimbali. 


Hatua Moja Baada ya Nyingine

Ingawa vita dhidi ya malaria bado haijamalizika, hatua zilizopigwa katika Mkoa wa Ruvuma zinaonesha kuwa mafanikio yanawezekana kupitia mshikamano wa jamii, usimamizi makini na mikakati ya kitaalamu. 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waridhia miradi yote Tunduru

    May 16, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waangaza Namtumbo

    May 15, 2025
  • AMEUONA Mwenge Songea baada ya miaka 63 ya Uhuru

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru watingisha Manispaa ya Songea,wapitia miradi ya bilioni 1.8

    May 14, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.