Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mheshimiwa Simon Chacha amezindua mradi wa visima 900 katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Ligunga ikiwa na matukio kuelekea kilele cha wiki ya maji kitakachofanyika Machi 22 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutekeleza kwa vitendo ajenda ya kumtua mwanamke ndoo kichwani.
Amesema licha ya Tanzania kubwa nchi kubwa,katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia ameleta mageuzi makubwa katika sekta ya maji ikiwemo Wilaya ya Tunduru.
Amewaasa wananchi kutunza miundombinu yam aji na miradi mingine inayotekelezwa ili iwe endelevu na kutumika katika kizazi cha sasa na kijacho.
Awali akitoa taarifa ya upatikanaji wa maji katika Wilaya hiyo,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tunduru Mhandisi Maua Mgallah amesema Tunduru ina vijiji 139 kati ya hivyo vijiji 20 tu ndivyo havina maji safi na salama hali iliyosababisha upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo kufikia asilimia 81.
Ameitaja miradi inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya hiyo ni kumi yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni 13.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.