• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI kuweka lami barabara ya Amanimakoro-Ruanda KM 35

Imewekwa kuanzia tarehe: October 27th, 2022

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)mkoa wa Ruvuma, imeanza ujenzi wa barabara la Amanimakoro-hadi Ruanda yenye urefu wa km 35 kwa kiwango cha lami  ili kurahisisha shughuli za usafiri  wa wananchi na usafirishaji wa  bidhaa mbalimbali.

Akizungumza  Meneja wa TANROADS  Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi alisema, barabara hiyo inajengwa na kampuni ya China Railway Sevent Group(CRSG) gharama ya Sh.bilioni 60.4 zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.

Alisema,barabara ya Amanimakoro-Ruanda ni ya kimkakati na muhimu sana kiuchumi kwa kuwa ndiyo inayounganisha wilaya ya Mbinga na Nyasa na inatumika kusafirisha makaa ya mawe kutoka kwenye migodi iliyopo kwenye vijiji vya wilaya ya Mbinga kwenda mikoa mingine hapa nchini na nchi jirani.

Alisema,barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Kitai-Ruanda hadi Lituhi kuelekea Mbambabay kupitia bandari ya Ndumbi,ambapo serikali iko katika maandalizi ya kujenga kipande kingine   kutoka Ruanda hadi bandari ya Ndumbi chenye urefu wa km 50 kwa kiwango cha lami.

Alisema, kwa sasa kazi ya ujenzi inaendelea vizuri na mategemeo ya serikali kwamba  itakamilika kwa mujibu wa mkataba ifikapo mwezi  Disemba mwaka 2023.

Alisema,itakapokamilika itatoa fursa kwa wananchi kuitumia barabara hiyo katika shughuli zao za maendeleo na kuwaomba wale wote wanaopitiwa na ujenzi wa mradi huo kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi na kutoa ushirikiano  kwa mkandarasi.

Kwa mujibu wa Mlavi ni kuwa, kuwepo kwa mradi huo kwenye maeneo yao ni fursa kubwa kwani utawawezesha kufanya shughuli mbalimbali na kupata kazi  ambazo zitawaingizia kipato.

Mlavi alisema wananchi hawana budi kutambua kwamba, barabara hiyo ni yao inajengwa kwa manufaa yao kwa hiyo wana wajibu wa kuitunza na kuhakikisha hakuna hujumu yoyote ikiwamo wizi wa vifaa vinavyoletwa kwa ajili ya mradi huo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Amanimakoro na Ruanda wilayani Mbinga, wameipongeza serikali ya awamu ya sita kuanza ujenzi wa barabara hiyo ambayo inakwenda kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika wilaya za Mbinga na Nyasa na Taifa kwa ujumla.

Halfani Omari mkazi wa kijiji cha Amanimakoro alisema,barabara hiyo itakapokamilika itasaidia kufanya shughuli zao za kiuchumi na kurahisisha usafiri kati ya kijiji hicho na  maeneo mengine ya wilaya ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma.

Aliongeza kuwa, kwa muda mrefu changamoto kubwa katika barabara hiyo ni vumbi la makaa ya mawe kuingia ndani ya nyumba zao pindi malori yanapopita, hivyo  kusababisha madhara  mbalimbali kama kukohoa  na mafua ya mara kwa mara.

Frolian Kayombo mkazi wa kijiji cha Ruanda alisema,kutokana na ubovu wa barabara hiyo, kumesababisha kupanda kwa gharama za maisha,kukosekana kwa usafiri wa uhakika na hata  bei bidhaa mbalimbali kuwa kubwa.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara June 30, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • UTARATIBU wa kupandisha hadhi barabara June 30, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA alivyodhamiria kuwekeza tena kwenye elimu ya sekondari

    March 24, 2023
  • CHIFU wa Tano wa kabila la wangoni Emanuel Zulu Gama

    March 24, 2023
  • MAABARA ya kisasa katika sekondari ya Lusonga Mbinga

    March 23, 2023
  • TUFANYE utalii wa ndani tusisubiri wageni kutoka nje

    March 24, 2023
  • Tazama zote

Video

RAIS SAMIA alivyomaliza kero ya maji Songea
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.