IElimu ya sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imepiga hatua mpya baada ya kusajiliwa kwa Shule ya Sekondari Amali Lundusi—shule ya kwanza na pekee kutoa elimu ya amali sambamba na elimu ya jumla, hatua inayotarajiwa kuibua kizazi cha wahitimu wenye ujuzi wa kujiajiri na kuchochea maendeleo ya jamii
.Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Bumi Kasege, amesema usajili huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuimarisha elimu inayojibu mahitaji halisi ya soko la ajira.Shule hiyo ilifunguliwa rasmi Januari 12, 2026 ikiwa na walimu wanane na wanafunzi 60 wa kutwa—wasichana 30 na wavulana 30—waliokwisha anza masomo.Kwa sasa, shule imeanza kutoa kozi ya Field Crop Production,
ikilenga kuwapa wanafunzi maarifa ya kisasa ya kilimo, sekta inayobeba uchumi wa eneo hilo.Katika hatua nyingine ya kupanua fursa za elimu, Shule ya Sekondari Mtopesi imepandishwa hadhi na itaanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano Julai 2026 baada ya kukamilika kwa mabweni mapya mawili.Wanafunzi wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusogeza elimu bora karibu na wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.