Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefanya uchunguzi wa lishe kwa watoto chini ya miaka mitano ambapo watoto 43,120 kati ya 45,000 sawa na asilimia 95.8 walifanyiwa tathmini. Matokeo yameonesha kuwa zaidi ya asilimia 99 wako kwenye hali nzuri ya lishe!
Mkurugenzi wa Manispaa, Wakili Bashir Muhoja, amezitaka idara za elimu na jamii kuimarisha utoaji wa chakula shuleni kuanzia Novemba 2025.
Zaidi ya shule 130 zimeanzisha bustani za lishe na kuelimisha wanafunzi kuhusu ulaji wa vyakula vyenye virutubishi
Sekta za kilimo, mifugo na uvuvi pia zimechangia mafanikio haya kupitia elimu, uzalishaji wa maziwa zaidi ya lita milioni 3.5, na kuku zaidi ya milioni 13
Songea inaendelea kuonesha mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya udumavu na utapiamlo kwa watoto na jamii kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.