Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, amepongeza ujenzi wa Jengo la TAKUKURU Wilaya ya Nyasa, Ruvuma, lililokamilika kwa ubora wa hali ya juu na ndani ya bajeti. Mradi huo umetumia shilingi milioni 224 pekee, na milioni 12 zikisalia — jambo adimu katika utekelezaji wa miradi ya umma nchini.
Jengo hilo, ambalo lingeweza kugharimu hadi milioni 500 katika maeneo mengine, limejengwa kwa uwazi, uadilifu na usimamizi makini wa timu ya TAKUKURU Nyasa. Mradi huo umetekelezwa kwa awamu mbili kupitia bajeti za 2022–2023 na 2024–2025, katika eneo la Kilosa Kati, Bomani, Wilaya ya Nyasa.
Chalamila alisisitiza kuwa mafanikio haya ni kielelezo cha utekelezaji bora wa Ilani ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema:
“Haki haitakiwi tu kutendeka, bali ionekane ikitendeka.”
TAKUKURU inaendelea kuthibitisha kuwa uadilifu unajenga taifa!

Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.