Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Louis Chomboko, amesema kuwa ukusanyaji wa takwimu sahihi na zenye ubora kuhusu hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano ni msingi wa mipango bora, maamuzi yenye ushahidi na utekelezaji wa afua madhubuti za lishe na afya ya mtoto.
Amesema hayo wakati wa akifungua mafunzo kwa watafiti wasaidizi kuhusu utafiti wa hali ya lishe mkoani Ruvuma yaliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Songea (HOMSO) yakiwajumuisha maafisa lishe, madaktari, wauguzi pamoja na waratibu wa huduma za maabara.
Dkt. Chomboko amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wataalam hao uwezo wa kitaalamu katika ukusanyaji wa takwimu sahihi. Akibainisha kuwa jukumu la watafiti wasaidizi ni nyeti na linahitaji uadilifu, umakini na weledi wa hali ya juu.
Amesisistiza kuwa ushiriki wa wataalamu wa maabara katika mafunzo hayo ni muhimu ili kuhakikisha vipimo vinazingatia viwango na miongozo ya utoaji huduma bora, madaktari na wauguzi watasaidia kuratibu huduma na kuhakikisha utafiti unaendana na mifumo ya huduma za afya iliyopo.
Vilevile amesema maafisa lishe watachangia katika kutoa mwelekeo wa kitaalamu kuhusu viashiria vya lishe. Hivyo, amewataka wataalamu hao kuwa makini na kujituma katika mafunzo hayo, akisisitiza kuwa baada ya mafunzo, zoezi la ukusanyaji wa takwimu za lishe kwa kila halmashauri litaanza rasmi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.