Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limewataka wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake watumie majiko ya kisasa ya umeme aina ya induction cooker na pressure cooker.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma, Alan Njiro, alisema katika kongamano la wafanyabiashara wadogo lililofanyika Songea Club kuwa tafiti zimeonyesha vifaa hivyo ni salama, vinapunguza gharama na hutumia umeme kidogo.
“Teknolojia imeboreshwa, majiko ya sasa yanapika haraka, ni nafuu na yanasaidia kuhifadhi mazingira,” alisema Njiro.
Alisisitiza wajasiriamali, hasa mama lishe, kutumia vifaa hivyo ili kuongeza tija kwenye shughuli zao na kuachana na vifaa vilivyopitwa na wakati.
Kupitia Mradi wa Ujazilizi, TANESCO imepanga kutoa elimu na maonyesho ya vifaa hivyo katika maeneo ya pembezoni ili wananchi wote wanufaike na matumizi ya umeme wa uhakika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.